Thursday, October 18, 2012


LIONESS WILDLIFE TRAINING CENTRE-KARATULIONESS WILDLIFE TRAINING CENTRE








Horizontal Scroll: MAISHA MWITU NI RASILIMALI
 





Office contacts: mobile: +2557 8616 4015                                                      11/10/2012
                                         +2557 6838 1469
                          Email: lionesswildlife@gmail.com
MWAALIKO KWENYE MDAHALO WA KITAALUMA JUU YA SIKUKUU YA KUMUENZI BABA WA TAIFA
LETU MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Husika na mada tajwa hapo juu, kwa kuzingatia umuhimu wa kuwaenzi viongozi mashuhuria na waliotumia nafasi zao katika kupigania haki, usawa na uhuru Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla, LIONESS WILDLIFE TRAINING CENTRE KARATU imeandaa mdahalo wa kitaaluma kwa lengo la kuwakutanisha wanavyuo wa Vyuo vya kati mbalimbali hapa karatu mjini wakiwa kama wataalam chipukizi wa taifa hili kujumuika pamoja na kujadili nafasi ya baba wa taifa katika maendeleo ya taifa letu, Afrika na Duniani kwa ujumla, katika Nyanja za Kihistoria, kiuchumi, kisiasa na kijamii. Mdahalo utafanyika siku ya jumapili tarehe 14/10/2012 ambayo ni siku aliyofariki dunia.
Muda wa mdahalo: 2:00 mchana hadi 4:00 jioni
Mahali: CHUO CHA LIONESS WILDLIFE TRAINING CENTRE
“MAENDELEO YA TAIFA HUCHOCHEWA NA WANATAALUMA WAZALENDO KWA KUREJEA MITIZAMO ZA WAASISI WA TAIFA”

MKUU WA CHUO LIONESS WILDLIFE TRAINING CENTRE
Mr Kisando Nina

No comments:

Post a Comment