Sunday, March 27, 2011

habari za loliondo kwa babu

Sun 27 Mar 2:4PM
Home Habari Habari za Kitaifa Serikali yaomba baraka za Mchungaji Loliondo
BOOKMARK THIS PAGE
Serikali yaomba baraka za Mchungaji Loliondo  Send to a friend
Thursday, 24 March 2011 21:36
0diggsdigg
Abiria wa basi la kukodi kutoka wilayani Nzega, wakisukuma gari lao lililokwama katika mpaka wa mbuga ya wanyama ya Serengeti na Loliondo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jumatano , walipokuwa wakielekea kijiji cha Samunge, mkoani Arusha kwa ajili ya kunjwa dawa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile.
Na Waandishi Wetu
KIKAO cha kutafuta njia bora ya kuwawezesha wananchi kupata tiba ya magonjwa sugu huko Loliondo kilichoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na viongozi wa mikoa sita wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdore Shirima na mwenzake wa Mara, Enos Mfuru kimeahirishwa katika kile kinachoaminika kuwa ni hadi pale maazimio yake yatakapopata baraka za Mchungaji Ambilikile Mwasapile.

Lukuvi aliwaambia waandishi wa habari mara baada ya kuahirisha kikao hicho saa 3:35 usiku kuwa bado kuna mambo ya kujadiliwa kabla ya kutoa tamko rasmi.“Kikao kimeahirishwa tumepeana majukumu, kesho Mkuu wa Mkoa wa Arusha atakuwa Loliondo kuongea na Mchungaji Ambilikile Mwasapile na kujionea hali ilivyo kwa sasa na wengine wamepewa majukumu mengine, hivyo kesho (leo) tutakuwa na la kuwaambia baada ya RC kurudi," alisema.

Kwa muda wa siku nzima viongozi hao walikuwa katika Ukumbi wa Ofisi namba 40 katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha, wakijadili hali ilivyo huko Loliondo hasa baada ya mvua kuanza kunyesha na kusababisha msongamano mkubwa magari.

Mbali ya viongozi hao, mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Serikali kutoka Mikoa ya Singida, Kilimanjaro, Manyara na Shinyanga, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga na vingozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati.

Habari zilizopatikana baada ya kikao hizo zinasema Serikali inakusudia kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, mahema ya kutosha ambayo yatakodishwa kwa wananchi wanaokwenda huko.

Pia Serikali imerejea ahadi iliyoitoa wiki kadhaa zilizopita ya kuandaa utaratibu wa kuwasaidia wagonjwa waliozidiwa kupata huduma haraka kwa kutumia gari la kubebea wagonjwa (ambulance) ambalo kwa sasa limeshindwa kufanya hivyo kutokana na baadhi ya watu kudai gari hilo linatumika kuwabeba vigogo badala ya wagonjwa wenye hali mbaya.

Taasisi yajitokeza kujenga vyoo, mahema
Taasisi ya kimataifa ya masula ya mazingira ya Solar Oven Society Africa, imetangaza mpango wa kuokoa  maisha ya watu na uharibifu wa mazingira katika barabara iendayo Kijiji cha Samunge kwa kutoa vyoo na gari la kubeba wagonjwa.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mwakilishi wa Taasisi hiyo hapa nchini, Profesa Solomon Mwenda alisema wamechukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa kuna tatizo la huduma muhimu kwa wagonjwa na uharibifu mkubwa wa mazingira katika eneo hilo ambalo pia ni mapito ya wanyamapori.

“Tumekwenda Samunge na tumeona hali ni mbaya sana na ni hatari kwa afya za watu. Tumekuta bado watu wanajisaidia porini, bado chupa tupu na uchafu mwingi unatupwa barabarani hovyo,” alisema Profesa Mwenda.

Alisema kazi ya vyoo itaanza Jumanne ijayo na kwamba kila baada ya kilometa moja kutakuwa na choo cha muda. Pia watatoa gari la kubeba wagonjwa, mifuko ya kutunza taka, mahema na maofisa wa mazingira.

Mpaka sasa hakuna hata choo kimoja kilichokamilika kujengwa wakati Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imekuwa ikivuna kiasi cha Sh 6.4.milioni kwa siku katika Kijiji cha Samunge.

Tayari halmashauri hiyo imetia kibindoni kiasi cha Sh 140.8 milioni kwa mwezi mmoja lakini hivi sasa kuna taarifa ya mgonjwa mmoja kuhara damu, kwa mujibu wa ripoti kutoka zahanati ya kijiji jicho.

Pato hilo linatokana na tozo la ushuru wa kila siku kwa magari yanayokwenda kwa Mchungaji Mwaisapile kwa ajili ya kupata tiba. Mabasi makubwa na malori yanatozwa Sh10,000 kila moja, mabasi madogo yanatozwa Sh5,000 na madogo Sh2,000 huku pikipiki zikitozwa Sh1,000.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka kijijini, hapo pamoja na pato hilo ambalo awali lilikuwa likikusanywa na kijiji hicho hali bado ni mbaya na uchafu umekidhiri kila mahali vinyesi, mikojo katika chupa za plastiki ni hali ya kawaida eneo hilo .

Hali inazidi kuwa mbaya kiafya kutokana na mvua ziloanza kunyesha huku misururu mirefu inayofikia umbali wa kilomita 28 na watu waoadiriwa kufikia 150,000 wakiwa wanasubiri kupata tiba. Msururu huo unaanzia katika Kijiji cha Mdito.
Wananchi waliokwama katika msururu huo wamekuwa wakihangaika kupata chakula na vinywaji kiasi kwamba kila abiria wanaopita kutoka Kijiji cha Samunge, wamekuwa wakiombwa maji ya kunywa bila kujali kama yametumiwa na wengine au la.

Kijiji cha Mdito chenye kaya zisizozidi 50 hivi sasa kina watu wanaokadiriwa kufikia 200,000 ambao hawana mahitaji muhimu kabisa, huku wengine kama hao wakipata walau huduma kidogo na hao ni wale walio katibu na Kijiji cha Samunge, umbali wa kilometa 10.

Wakati huohuo; mvua zinaendelea kunyesha wilayani Ngorongoro hali ambayo inatishia uharibufu wa barabara.

Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali alisema kuwa kutokana na mvua hizo, ukarabati wa barabara ambao ulikuwa unafanywa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) umesitishwa kwa muda.

“Ni kweli barabara ni mbaya kutokana na mvua, watu wa Tanroads walikuwa wanatengeneza barabara ila nadhani sasa imekuwa kazi ngumu kwani mvua zimewakuta,” alisema Lali.

Tangu kuanza kwa mvua hizo takriban wiki moja sasa, mamia ya watu na magari wamekwama katikati ya Kijiji cha Selela na Ngaresero kutokana na mito kujaa na maeneo mengi kuharibika.

Lipumba aiponda Serikali 
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameishukia Serikali kwa kuruhusu tiba hiyo bila kufanyiwa uchunguzi na mkemia wake mkuu.

Lipumba ambaye hata hivyo, katika maelezo hayo hakuwakatisha tamaa wananchi kwenda kupata tiba hiyo, alisema kiutaratibu, watu hawazuiliwi kufanya tiba, lakini dawa lazima zipite kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili athibitishe ubora wake kabla ya kuruhusu watu waanze kuitumia.

Profesa Lipumba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Viwanja vya Zakheim, Mbagala Dar es Salaam.

"Katiba yetu haizuii mtu kuendesha shughuli za tiba, lakini taratibu ni kwamba tiba lazima ithibitishwe na maabara za Serikali. Ukiona Serikali inawaruhusu watu kutumia tiba bila kufuata utaratibu huo ujue imekwama," alisema.

Ingawa Lipumba hakutaja moja kwa moja tiba ya Loliondo, tiba iliyoanza kutolewa katika siku za hivi karibuni na kuibua mjadala mkubwa miongoni mwa jamii ni ile inayotolewa na Mchungaji Mwasapile.

Profesa Lipumba aliponda uamuzi wa Waziri Lukuvi kushinikiza tiba hiyo itolewe bila vipimo akisema ni sawa na kuhalalisha mambo yaendee kiholela katika nchi ambayo imejiwekea utaratibu wake kisheria.

"Waziri wa afya alikuwa sahihi sana kutaka dawa hiyo ipimwe kwanza, lakini Lukuvi akapingana naye, hii ni dalili mbaya kwa Serikali," alisema.

Habari hii imeandaliwa na Filbert Rweyemamu, Moses Mashala, Emanuel Herman, Arusha na Kizitto Noya.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Saturday, 26 March 2011 08:36
 

Comments 

 
0 #77 sikitiko kijaa 2011-03-26 06:27
Quoting popobawa:
Quoting sikitiko kijaa:
Quoting Kiroba:
Ni kwli sikitiko.Askofu Pengo ualiongea vzr ila watu hawataki kumsikiliza. badae yatatutokea puani.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alilieleza gazeti hili Kua:"Miujiza haiji kwa urahisi hivyo na watu kuponya kiasi hicho, huenda wanaweza kuponywa kwa ‘Illusion’ na baade ikaleta madhara."

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo Alisema cha msingi watu wanapaswa kuwa makini na serikali pia kwa sababu, wingi wa watu kuponywa huenda baadaye ukaleta vifo vingi zaidi kutokana na dawa yenyewe.

Pengo alisema: “Ninachoamini miujiza haiji kwa urahisi na watu wakaponywa kiasi hicho kwa mara moja, huenda ikawa ni kuponya kwa ‘illusion’ na baadae watu wakapata madhara makubwa.

“Ila sina jibu la kutoa kuhusu uponyaji huo, nabaki tu kushangaa na yanayotendeka kwa Mchungaji huyo hadi kufikia watu kuamini kiasi hicho,”alisema. Pengo alisema huenda akawa ameamua kutumia njia hiyo akawavuta hata wa waumini waingie kwenye imani yake na kuacha dini zao.

Safi kiroba kwa kutukumbusha haya


Tusikilize na ya askofu pengo nae. kidini huyu ndo kiongozi mkubwa kuliko wote tanzani. nasaha zake msumari

Quoting Pengo Jr:
71 KKKKKKKKK-Mganga ana utaratibu wake na haitaji kufuata busara zako.
#60 Rehema-Nilikaribia kukubaliana nawewe ila sijaona connection na shetani hapo. Hakuna concrete point kuunganisha na shetani.
#53 shebby-Just a mere assumption. Unataka tuamini ama tukubali?
#47 kunicha-Usimuite babu tapeli kwakuwa hafanyi unavyotaka wewe please.
#45 abdy-Huna fact za msingi. Hata neno can be dawa. Sio kikombe tu.
#34 kiongozi-Hoja za Pengo ni pumba tupu-Zako nzuri ziko wapi?
#23 Embu-Pengo hana mkate wowote. Hana dhiki kama wewe. Amesema hana uhakika na uponyaji wa watu wengi kama hivyo. Sio kaponda.
#18 msema kweli daima-I guess akili na ushujaa wako ni kuumwa na sioni busara kwako.
#16 MWANAMDODO-Sio lazima wote tuamini. Tumia busara
Pengo alisema ““Ila sina jibu la kutoa kuhusu uponyaji huo, nabaki tu kushangaa na yanayotendeka kwa Mchungaji huyo hadi kufikia watu kuamini kiasi hicho” Hakuponda, hakukataa.



Pengo jr soma hoja nzima ya kadinali Pengo. usisome mstari mmoja halafu ukatoa conclusion. wewe unasema Pengo hajampinga babu. Je aliposema:"Miujiza haiji kwa urahisi hivyo na watu kuponya kiasi hicho, huenda wanaweza kuponywa kwa ‘Illusion’ na baade ikaleta madhara" alikua anamsapoti
Quote
 
 
0 #76 Mabinza 2011-03-26 06:14
Quoting NGOSHA:
NDUGU YANGU HUTAKI KUKUBALI UKWELI KUWA ZITO NDIYO NGOME PEKEE YA CHADEMA AMBAYO WATU WANAOPENDA VIONGOZI BORA WANALITAMBUA HILO.

HAO VIONGOZI WENGINE WATU WANAWASAPOTI KWA USHABIKI WA UKABILA TU,MIMI NILIPIGIA KURA MBUGE WA CHADEMA LKN SIO KWA RAISI MAANA TUNAJUA WANACHAMA WA CHADEMA ASILIMIA KUBWA NI WACHAGA KWA AJILI YA UKABILA NA UDINI INGAWA MIMI NI MKRISTO DAMU ILA SIWEZI KUSAPOTI HAWA WAHUNI MBOWE NA SLAA KUTUGAWA WATAKAO FAIDIKA NI WACHAGA TUMEONA HAWA WACHAGA NA WAARUSHA HATA WALE WA CCM ASILI YAO NI UBINAFSI,WIZI NA UFISADI KWA UJUMLA SISI WASU[NENO BAYA] HAWATOTUKUMBUKA ILA WANATAKA KUTUTUMIA KAMA BIDHAA YA KUKIMBILIA IKULU MAANA NYERERE ALISHASEMA HATOINGIA MCHAGA AU MUARUSHA IKULU ALIKUWA ANAWAJUA HAWA MAOPPORTUNISTY WAPO TAYARI KUMWAGA DAMU ILIWAINGIE IKULU.

KAULI ZA UCHOCHEZI WATU WAFANYE VURUGU ILITANZANIA IGEUKE MISRI AU LIBYA NI UVUNJIFU WA SHERIA NA UCHOCHEZI WA KUVURUGA AMANI,
KAULI YA KUSEMA WANACHAMA WAVAMIE KITUO CHA POLISI KUWATOA VIONGOZI WA CHADEMA NI UVUNJIFU WA SHERIA NA AMANI.

KAULI YA NCHI HAITOTAWALIKA VIONGOZI WA CHADEMA WAKITA NI KAULI MBAYA SANA.

KAULI YA BAADA KUSHINDWA UCHAGUZI YA SLAA KUSEMA HAMTAMBUI RAISI NI DHAHIRI UCHU WA MADARAKA UMEWEKWA MBELE KULIKO MASLAHI YA WANANCHI,YOTE HAYO NI DHAHIRI KUWA CHADEMA HAKIPO KWENYE MASLAHI YA UMMA.
KILA MTANZANIA ANACHUKIA MAFISADI WA CCM LKN HATUWEZI KUWANYIMA KURA MAFISADI HALAFU TENA TUWAPE MAFISADI WENGINE NA WAHUNI.
ZITO KABWE WEWE NI JINIAZI WANAKUPINGA NI DHAHIRI MASHABIKI WA UKABILA WAPO PALE KWA AJILI YA MBOE NA SLAA KWA KUWA NI WAKABILA LAO.


Ni kweli Ngosha.
Quote
 
 
-1 #75 Pengo Jr 2011-03-26 02:42
71 KKKKKKKKK-Mganga ana utaratibu wake na haitaji kufuata busara zako.
#60 Rehema-Nilikaribia kukubaliana nawewe ila sijaona connection na shetani hapo. Hakuna concrete point kuunganisha na shetani.
#53 shebby-Just a mere assumption. Unataka tuamini ama tukubali?
#47 kunicha-Usimuite babu tapeli kwakuwa hafanyi unavyotaka wewe please.
#45 abdy-Huna fact za msingi. Hata neno can be dawa. Sio kikombe tu.
#34 kiongozi-Hoja za Pengo ni pumba tupu-Zako nzuri ziko wapi?
#23 Embu-Pengo hana mkate wowote. Hana dhiki kama wewe. Amesema hana uhakika na uponyaji wa watu wengi kama hivyo. Sio kaponda.
#18 msema kweli daima-I guess akili na ushujaa wako ni kuumwa na sioni busara kwako.
#16 MWANAMDODO-Sio lazima wote tuamini. Tumia busara
Pengo alisema ““Ila sina jibu la kutoa kuhusu uponyaji huo, nabaki tu kushangaa na yanayotendeka kwa Mchungaji huyo hadi kufikia watu kuamini kiasi hicho” Hakuponda, hakukataa.
Quote
 
 
0 #74 kanchi 2011-03-26 00:34
TUNATAKA SHUHUDA PIA JAMANI WALIOKWENDA KWA BABU ILI TUWEZE KUAMINI VIZURI KAMA INAFANYA KAZI YA UPONYAJI.
Quote
 
 
0 #73 PETER PASCAL 2011-03-25 22:03
Watanzania tuache fitina babu anatibu. Tuache kusema maneno ya uongo
Quote
 
 
0 #72 Julius Dominic 2011-03-25 22:00
Pro Lipumba unapoteza muda kuzungumzia dawa ya Loliondo wakati kuna mambo mengi mabaya yanafanywa ma serikali unashindwa kuyasema?Au ndiyo muungano wako na CCM unafanya kazi nzuri sasa?Vua joo la CUF vaa la CCM watu tujea kabisa hutakuwa wa kwanza kufanya hivyo,Pro Lipumba hali ya nci ni mbaya achana na habari za Loliondo zungumzia hali inayoikabiri nchi.
Quote
 
 
+2 #71 KKKKKKKKK 2011-03-25 20:22
INGEKUWA VEMA KAMA KWELI HUYO MZEE ANA DAWA, AKAANDAA UTARATIBU WA KUWAFUATA WAGONJWA HOSPITALINI.

NI RAHISI KUMSAFIRISHA YEYE MIKOA MBALIMBALI, KULIKO WATANZANIA WOOOOOOOTE WAMFUATE YEYE HOKO LOLIONDO!

SERIKALI HAIJATUMIA BUSARA KATIKA HILI!

SHERIA ZA AFYA NA USALAMA WA RAIA ZINAKANYAGWA - KWA VILE HAKUNA ANAYESIMAMIA SHERIA TANZANIA.

HIVI KWELI KILA MTU AKIFANYA HIVI TUTAISHIJE WATANZANIA?

KESHO MWINGINE AKITUAMBIA YESU YUKO KATIKATI YA BAHARI YA HINDI TUTAKIMBILIA HUKO?

KAMA MTU ANA DAWA, AFUNGUE ZAHANATI NA HOSPITALI ZAKE KWA KUFUATA UTARATIBU JAMANI.

TUTAACHAJE KUAMINI KUWA WATU WANAENDA KUTAFUTA MADARAKA KWA WACHAWI, WAGANGA WA KIENYEJI NA WANAJIMU?
Quote
 
 
+1 #70 kIDONGOI 2011-03-25 19:05
wacheni kutuaibisha jamani! Huku nje tunaulizwa maswali ya kebehi! yaani dunia hii yenye sehemu takatifu za kikristo, yenye papa, makardinali n.k. wasioteshwe akaoeshwe m[NENO BAYA] wa Loliondo! Huyu Lukuvi simshangai ni mtu wa totoz toka akiwa umoja wa vijana. Miwaya hakosi ndio maana anavu[NENO BAYA] na tiba ya babu! Kwanza ana nyodo hata ofisini kwake ukiingia anakutazama kuanzia miguuni hadi utosini kama vile namsumbua! Anachagua wtu wa kuwapa mkono wengine anakupa vidole viwili uvishike usimchafue! Huyo ni mtu wa hovyo na watu wenye akili zao hawawezi kufuata mawazo yake.
Hili dili nyie subirini tu litabumburuka muda si mrefu. Serikali itaingia aibu ya mwaka kwa kuwa inaingilia kitu cha hovyo. Serikali imetoa kibali kila anayeota sasa atibu watu! Serikali ya hovyo kabisa! Eti inaogopa kuchukiwa na walokole! kwani sasa wanaipenda serikali! Serikali inayotafuta baraka za mtu aliyeota! Kha! Inatia kichefuchefu. Jamani, uchauzi ujao chagueni mtu makini. Mkichagua mhuni mtapata mambo ya kihuni kama haya. Ingekuwa mwalimu yupo hai akiwatia bakora hao japokuwa ni wakristu wenzie.
Quote
 
 
+4 #69 helena 2011-03-25 17:56
mimi naogopa watu wanaposema dawa ya babu ipimwe hivi kweli itakapopimwa dawa ya babu na kukutwa ni sumu au ina madhara yeyote ni nani atasubutu kutangaza wakati viongozi wa ngazi za juu karibu wote wamehudhuria kupata kikombe? na ni kwa nini wasijitokeze wagonjwa waliopona wakashuhudia kwenye vyombo vya habari wakiwa na vyeti vyao! kwa nini serikali haitaki kufuatilia vizuri suala la babu au kuna siri gani kati ya serikali na babu?
Quote
 
 
-1 #68 jahman 2011-03-25 17:50
Quoting sendaro:
dawa za babu Ambbilikile zinatibu vizuri asiye pona kwa ndawa hiyo ajue ni FISADI. haiingii akilini watu wote wanaoenda loliondo ni [NENO BAYA], kwani katangaza kwenye tv au redio c wameenda wenyewe? himahima watanzania msisikilize maneno ya wa2 twendeni tukapate kikombe cha
babu........

mnatuchanganya babu anatibu au anaponya tucheck kamusi hakafu mtuweke wazi...
Quote
 
 
+2 #67 heavenlight 2011-03-25 17:32
kama mtu anaandika comment atoe comment kwa ajili ya kushauri na si kuandika tuu kwa sababu kuna nafasi ya kuandika. pia lugha za [NENO BAYA] zinadhihirisha jinsi watanzania tusivyo heshimu mawazo na kazi za watu wengine. pia kuhusu babu, kama dawa ya babu ni mpango wa mungu itadhihirika na kama si mpango wa mungu pia itadhihirika pia kusema babu ni wakala wa shetani ni kuwa na kiwango kidogo cha kufikiri. watanzania tuwe makini sana na maoni tunayotoa
Quote
 
 
+2 #66 DESRE 2011-03-25 16:26
WIZI MTUPU....WATZ BADO HATUJAELIMIKA KABISA,,,,,,,,A F NAMNA HII NDIO WATU WAWE NA TAMAA YA KUWATOA CCM MADARAKANI KAMA ASILIMIA KUBWA YETU TUPO HIVI
Quote
 
 
-1 #65 Mahmod 2011-03-25 16:05
HIVI MBONA MNAMSAKAMA BABU WA WATU? NANI ALIMTANGAZA HUYU BABU KUTOKA HUKO POLINI? NAFIKIRI NI WATU WALIOPONA.kUNA WAGANGA WANGAPI WANALIPIA GHARAMA KUBWA KWENYE TV NA REDIO KUJITANGAZA NA HAWAJAPATA POPULARITY KAMA HII.WANAOKEBEI HAWAJAWAHI LALA KINDANI MWEZI MMOJA KWA UGONJWA.Quoting shebby:
HII DAWA YA BABU HAINA MSINGI WOWOTE NA UHUSIANO WA MAGONJWA ANAYOJIDAI KUTIBU, INAWEZEKANA KABISA HAPA KUNA GAME LINACHEZWA KUWAPUMBAZA WATZ NA MATATIZO YANAYOTUSIBU
Quote
 
 
0 #64 vuvulzela 2011-03-25 15:49
Mhariri wa Mwananchi tunaomba muiweke habari ya Naibu waziri wa elimu "Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, Serikali ina taarifa kuwa, baadhi ya wahadhiri wanatumia muda wa kutoa mihadhara ya masomo kwa kuzungumzia siasa hasa kupiga vita Serikali iliyopo madarakani" ili tumchambue.

Please hii habari ilikuwa katika gazeti la Habari leo tuesday or wednesday. Weka ukulasa wa juu ili aone kuna comments ngapi maana wanasoma
Quote
 
 
-4 #63 Mnyonge Mnyongeni... 2011-03-25 15:11
Quoting NGOSHA:
NDUGU YANGU HUTAKI KUKUBALI UKWELI KUWA ZITO NDIYO NGOME PEKEE YA CHADEMA AMBAYO WATU WANAOPENDA VIONGOZI BORA WANALITAMBUA HILO.

HAO VIONGOZI WENGINE WATU WANAWASAPOTI KWA USHABIKI WA UKABILA TU,MIMI NILIPIGIA KURA MBUGE WA CHADEMA LKN SIO KWA RAISI MAANA TUNAJUA WANACHAMA WA CHADEMA ASILIMIA KUBWA NI WACHAGA KWA AJILI YA UKABILA NA UDINI INGAWA MIMI NI MKRISTO DAMU ILA SIWEZI KUSAPOTI HAWA WAHUNI MBOWE NA SLAA KUTUGAWA WATAKAO FAIDIKA NI WACHAGA TUMEONA HAWA WACHAGA NA WAARUSHA HATA WALE WA CCM ASILI YAO NI UBINAFSI,WIZI NA UFISADI KWA UJUMLA SISI WASU[NENO BAYA] HAWATOTUKUMBUKA ILA WANATAKA KUTUTUMIA KAMA BIDHAA YA KUKIMBILIA IKULU MAANA NYERERE ALISHASEMA HATOINGIA MCHAGA AU MUARUSHA IKULU ALIKUWA ANAWAJUA HAWA MAOPPORTUNISTY WAPO TAYARI KUMWAGA DAMU ILIWAINGIE IKULU.

KAULI ZA UCHOCHEZI WATU WAFANYE VURUGU ILITANZANIA IGEUKE MISRI AU LIBYA NI UVUNJIFU WA SHERIA NA UCHOCHEZI WA KUVURUGA AMANI,
KAULI YA KUSEMA WANACHAMA WAVAMIE KITUO CHA POLISI KUWATOA VIONGOZI WA CHADEMA NI UVUNJIFU WA SHERIA NA AMANI.

KAULI YA NCHI HAITOTAWALIKA VIONGOZI WA CHADEMA WAKITA NI KAULI MBAYA SANA.

KAULI YA BAADA KUSHINDWA UCHAGUZI YA SLAA KUSEMA HAMTAMBUI RAISI NI DHAHIRI UCHU WA MADARAKA UMEWEKWA MBELE KULIKO MASLAHI YA WANANCHI,YOTE HAYO NI DHAHIRI KUWA CHADEMA HAKIPO KWENYE MASLAHI YA UMMA.
KILA MTANZANIA ANACHUKIA MAFISADI WA CCM LKN HATUWEZI KUWANYIMA KURA MAFISADI HALAFU TENA TUWAPE MAFISADI WENGINE NA WAHUNI.
ZITO KABWE WEWE NI JINIAZI WANAKUPINGA NI DHAHIRI MASHABIKI WA UKABILA WAPO PALE KWA AJILI YA MBOE NA SLAA KWA KUWA NI WAKABILA LAO.

Jamani mimi nilidhani ni Magazeti (Print) tuu huwa yanachelewa kuwafikia wasomaji, sikujua kuwa hata web pages huwa zinachelewa pia, maana it looks like mwenzetu anasoma gazeti la mwezi uliopita.. this is worth looking into, or it could be ndiyo amefunga modem yake hivyo ameanzia kwenye ARCHIVES, strangely comments came to the wrong forum of comments.. TECHNOLOGY!!!!!
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!



7000 symbols left


Security code
Refresh


  • Kupiga Kura

  • Jumapili


Nini ukweli wa Dawa ya magonjwa sugu ya Mchungaji Ambilikile wa Loliondo?