Monday, August 27, 2012

NEWS, 27, AUG,2012

UZINDUZI WA MRADI WA TOA TAARIFA UWE SALAMA BARABARANI JIJINI MWANZA


Mtendaji Mkuu naMkurugenziMtendaji wa Benki  ya Posta Tanzania (TPB)Sabasaba Moshingi,mwenye suti ,akiteta jambo na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani ,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa polisi (SACP)Mohamed Mpinga,kabla ya kuzindua mradi wa Toa Taarifa Uwe Salama Barabarani
Picha na Mashaka Baltazar wa Fullshangwe. Mwanza

Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga, kulia akiwa katika picha ya pamojanaMtendaji Mkuu na Mkurugebnzi wa Benki ya Posta,Sabasaba Moshingi,wa tatu kutoka kulia,wa pili ni Liberatus Barlow,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza na kushoto wa kwanza, ni Kamanda wa kikosi cha  usalama barabarani Mkoa wa Mwanza, SP Nuru Selemani katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa Toa taarifa Uwe Salama barabarani.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani, Kamishna Msaidizi mwandamisi wa polisi (SACP) Mohamed Mpinga, akitoa ufafanuzi wa jambo kwa waandishi wa habari jijini Mwanza (hawapo pichani ) kabla ya kuzindua mradi wa Toa Taarifa Uwe Salama.Katikati ni  Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, ACP Liberatus Barlow na kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu na Sabasaba Moshingi  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ambayo imefadhili mradi huo kwa shilingi milioni 30.
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani ,Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP ) Mohamed Mpinga wa kwanza kulia, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza ,Kamishna Msaidizi (ACP) Liberatus Barlow ( wa pili kutoka kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi mwenye suti,wakiwa wameshika bango lenye namba za kudumu za Makamanda wa vikosi vya Usalama barabarani wa mikoa ya Kanda ya ziwa, zitakazotumika kutoa taarifa kwa jeshi hilo ,kuhusu ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani unaofanywa na madereva wa magari ya abiria.Katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika kituo kikuu cha mabasi Nyegezi na kuhudhuriwa na maofisa wa jeshi la polisi

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani, SACP Mohamed Mpinga akiwaelekeza abiria jinsi ya kutumia namba za kamanda wa vikosi vya usalama barabara,wakati madereva wanapokiuka kanuni na sheria za usalama barabarani wawapo safarini .Abiria wanapaswa kutoa taarifa kupitia namba hizo za simu  ambao zitakuwa hewani  kwa saa 24.Mpinga alikuwa akizindua mradi wa Toa taarifa Uwe salama unaofadhiliwa na Benki ya posta nchini kwa shilingi milioni 30.

Kamanda Barlow akielekeza  jambo namna ya kutumia namba za kudumu za  RTO wa mikoa yan kanda ya Ziwa  zilizopo kwenye bango lililobandikwa ndai ya basi la abiria katika kituo cha mabasi Nyegezi muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa Toa Taarifa uwe Salama,mradi unaofadhiliwa na Benki ya Posta Tanzania kwa ajili ya kupunguza na kutokomeza ajali za barabarani  nchini.

DIWANI KWADELO, KONDOA AHAMASISHA MAENDELEO KIAINA


Wakazi wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, wanakabiliwa na uhaba wa maji safi na salama kwa zaidi ya miaka 20 sasa, kutokana na miundombinu iliyozinduliwa mwaka 1973, na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere,  wakati wa uhai wake,  kufa kwa kukosa uangalizi.
Diwani wa Kata hiyo, Omary Kariati (wapili kulia) na Msaidizi wake  Bakari Ndee wakionyesha tangi la maji lililozinduliwa na Baba wa Taifa ambalo sasa halifanyi kazi. Diwani alionyesha tangi hilo,  wakati wa harambee ya kuchangisha fedha za kufufua mradi wa maji. Sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana. Pia gunia 37 za alizeti zenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe zilichangwa kwa ajili hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo. 
Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati akiendesha trekta wakati akiwasili kwenye hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji katika kata hiyo, jana. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Kushoto ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo. .

Trekta 64 za wakulima wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, ambazo wamezipata kwa jitihada za diwani wa kata hiyo, Omary Kariati kutoka Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT, zikiwa zimeegeshwa eneo la mkutano ulioitishwa na diwani huyo, kwa ajili ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji wa kata hiyo, jana. Wakulima hao walifika na trekta hizo na kuwa mstari wa mbele kuchangia mradi huo wa maji.  Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Wananchi wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, wakiwa kwenye mkutano wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji, katika kata hiyo, jana. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 1012 LAFANA UWANJA WA MKWAKWANI TANGA

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego pichani kati mwenye kipaza sauti akisoma namba za washindi waliojinyakulia piki piki mbili zilizotolewa na kampuni ya Push Mobile,wa tatu kulia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile,Rugambo Rodney na mwisho kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga,na nyuma kabisa ni Mkurugenzi wa utafiti Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Ephrahim Mafuru wakishuhudia tukio hilo usiku huu kwenye uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linafanyika.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga usiku huu mara baada ya kuwataja washindi waliojishindia piki piki mara baada ya kuchezeshwa bahati nasibu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea,pichani kati ni Afisa Mahusiano wa Clouds Media Group, Simon Simalenga.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuru akitumbuiza jukwaani usiku huu na shabiki wake mbele ya wakazi wa jiji la Tanga wanaondelea kutiririka ndani ya uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linafanyika.
Msanii kutoka THT,ajae kwa kasi katika anga ya muziki wa bongofleva aitwaye Rachel akiimba jukwaani usik
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuru akitumbuiza jukwaani usiku huu na shabiki wake mbele ya wakazi wa jiji la Tanga wanaondelea kutiririka ndani ya uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linafanyika.
Msanii kutoka THT,ajae kwa kasi katika anga ya muziki wa bongofleva aitwaye Rachel akiimba jukwaani usiku huu.
uru akiimba kwa manjonjo na shabi wake jukwaani usiku huu.
Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua ngoma 
Sehemu ya umati wa wakazi wa Tanga wakifuatilia kwa makini makamuzi ya Fiesta usiku huu.
<div

Mageni asaidia ujenzi kituo cha afya Hungumalwa Kwimba

Mkufunzi Emmanuel Mageni (kushoto) akikabidhi msaada wa mifuko 10 ya saruji kuchangia ujenzi kituo cha afya katika Kata ya Hungumalwa wilayani Kwimba, jana. Na Mpiga Picha wetu
Na Mwandishi wetu, Kwimba
MATUMAINI ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Hungumalwa wilayani Kwimba, Mwanza, yameongezeka baada ya Mkufunzi wa Chuo cha Ualimu Murutunguru wilayani Ukerewe, Emmanuel Mageni, kuchangia mifuko 10 ya saruji.
Mageni alikabidhi mchango wake huo kwa uongozi wa kata hiyo jana, ikiwa ni miezi minne tangu alipotoa ahadi ya kusaidia ujenzi huo katika harambee iliyoongozwa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Kangoye.
Mageni, ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alitoa msaada huo baada ya kuguswa na ukubwa wa tatizo la ukosefu wa huduma za afya za kitaalamu linaowakabili wakazi wa kata hiyo kwa muda mrefu.
Akikabidhi msaada huo jana, Mageni alitumia fursa hiyo kumpongeza Diwani wa Kata ya Hungumalwa, Shija Malando, kwa kubuni na kuhamasisha ujenzi wa kituo hicho cha afya huku akimhimiza kuongeza juhudi zaidi katika kushughulikia maendeleo ya wananchi.
“Ninakupongeza (Malando) kutokana na juhudi kubwa unazofanya katika kutafuta maendeleo ya wakazi wa Kata ya Hungumalwa, matumaini yangu ni kwamba wananchi wataendelea kukuunga mkono katika jitihada za kujiletea maendeleo,” alisema Mageni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo hicho cha afya, John Nkumba, alisema ujenzi huo ulianza mwaka jana kutokana na michango mbalimbali ya wananchi, ambapo kwa sasa umefikia hatua ya linta ukiwa umekwisha kugharimu zaidi ya sh. milioni 10.
Ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kuwaondolea wakazi 14,168 matatizo ya vifo visivyo vya lazima, wajawazito kujifungulia njiani na adha ya kutembea umbali wa kilomita 40 kwenda kutafuta matibabu wilayani Misungwi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Hungumalwa, Maneno Shaban, alimshukuru Mageni kwa kutekeleza ahadi hiyo akisema ni mfano mzuri unaopaswa kuigwa na wengine katika kuchangia maendeleo ya jamii.
Aidha, alimwomba Mageni kutosita kurudi katani hapo kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya pamoja na huduma za afya zitakazokuwa zinatolewa baada ya ujenzi huo kukamilika.

Wateja wafurahia Smirnoff Vodka na Smirnoff Ice katika promosheni ya Mbalamwezi Beach Club

Mkurugenzi mpya wa kampuni ya bia ya Serengeti Bwana Steve Gannon wa pili kutoka kushoto akisakata disko ndani ya Mbalamwezi beach club wakati wa promotion ya Smirnoff vodka na Smirnoff ice.

Mkurugenzi mtendaji mpya wa kampuni ya bia ya Serengeti Steve Gannon akikabidhi zawadi ya T-shirt ya Smirnoff kwa mmoja wa washindi wa zawadi zilizotoilewa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji cha Smirnoff katika promosheni hiyo ya Smirnoff .
Meneja wa kinywaji cha Smirnoff Bi Azda Amani katikati akikabidhi zawadi ya T-shirt kwa mwanadada aliyejishia zawadi hiyo kwa kucheza vizuri katika promosheni hiyo ya Smirnoff .

RAIS KIKWETE NA FAMILIA YAKE WAHESABIWA KATIKA SENSA YA WATU NA MAKAZI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mama Salma Kikwete na familia yake  akijibu maswali toka kwa karani wa sensa ya wazu na makazi Bw. Clement Ngalaba leo Agosti 26, 2012wakati alipojiunga na mamilioni ya Watanzania katika zoezi hilo lililofanyika kwa mafanikio makubwa nchi nzima.
PICHA NA IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mama Salma Kikwete na familia yake  akijibu maswali toka kwa karani wa sensa ya wazu na makazi Bw. Clement Ngalaba leo Agosti 26, 2012wakati alipojiunga na mamilioni ya Watanzania katika zoezi hilo lililofanyika kwa mafanikio makubwa nchi nzima.

MDAU JANE KATUTUMIA PONGEZI ZAKE


Mdau Jane akiwa amepozi katika picha, Jane anawasalimia wadau wote wa  www.fullshangweblog.com  na anasema waendelee kutembelea mtandao huu kwani unafanya kazi nzuri ya kupasha habari katika jamii yetu, lakini pia anasema anafurahishwa na uboreshaji wa ukurasa wa fullshangweblog kwakuwa hivi sasa picha zinaonekana kwa ukubwa mzuri na zinavutia sana tofauti na ilivyokuwa awali.

MISS EAST AFRICA 2012 KURUSHWA “LIVE” NA M-NET AFRICA

Miss East Africa Seychelles-Annabelle Marvel Pointe (19)
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yataonyeshwa LIVE kupitia Mnet ambapo yanatarajiwa kutuizamwa na watu wanaokadiliwa kufikia million 200 kupitia televison na kwa njia ya internet Dunia nzima. 
Aidha maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea kwa kasi ambapo yamepangwa kufanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City,  jijini Dare s salaam, Tanzania badala ya mwezi September kama ilivyokuwa imetangazwa awali ili kutoa muda zaidi kwa Ncgi ambazo hazijapata wawakilishi wao kuweza kukamilisha zoezi hilo. 
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake ambapo yatashirikisha warembo kutoka katika Nchi 16 za ukanda wa afrika mashariki.

Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius. 
Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika  
Tayari baadhi ya Nchi zinazoshiriki mashindano hayo zimeshatangaza wawakilishi wake ambazo ni Eritrea, Ethiopia, Uganda, Southern Sudan, Malawi na Seychelles. Nchi zilizosalia zinatarajiwa kutangaza wawakilishi wao kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni tarehe 28 mwezi September. 
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,

Miss East Africa Uganda-Ayisha Nagudi (23)

Miss East Africa Ethiopia-Lula Teklehaimanot (19

Miss East Africa Eritrea-Rahwa Afeworki (22)

TANZANIA YAITAKA MALAWI KUSITISHA UTAFITI KATIKA ZIWA NYASA, YASISITIZA MAZUNGUMZO LICHA YA NCHI HIYO KUENDELEA NA MSIMAMO WAKE JUU YA UMILIKI WA ZIWA HILO

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akisalimiana na Rais Joyce Banda wa Malawi wakati walipokutana kwenye mkutanoa wa SADC nchini Msumbiji hivi karibuni
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 Lilongwe, MALAWI.
Tanzania imeitaka Malawi kusitisha shughuli za utafiti katika eneo la ziwa Nyasa lenye mgogoro  na kusisitiza nia yake ya kuendelea kuzungumza na nchi hiyo kuhusu mgogoro wa mpaka licha ya nchi hiyo kuendelea na msimamo wake wa kumiliki eneo lote la ziwa hilo.
Hayo yamebainishwa katika  mkutano wa wataalam na viongozi kutoka serikali ya Malawi na Tanzania kushindwa kufikia muafaka uliokusudiwa kuhusu eneo halali la mpaka unaotenganisha nchi hizo.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao cha usuluhishi kilichohusisha  timu za wataalam na viongozi wa wizara husika wa nchi hizo kilichomalizika  jana usiku mjini Lilongwe Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Bernard Membe amesema Tanzania bado inaamini katika mazungumzo ili kufikia muafaka wa kudumu wa mgogoro huo.
Amesema kuwa pamoja na sababu mbalimbali zilizotolewa na upande wa serikali ya Malawi juu ya umiliki wa eneo lote la ziwa Nyasa ,msimamo wa Tanzania juu ya mpaka unaozitenganisha nchi hizo uko wazi  kwa kwa kuzingatia vielelezo vya historia vilivyoachwa na wakoloni na sheria za kimataifa kuhusu mpaka kuwa katikati ya ziwa hilo.
Continue reading →

TAMASHA LA KUKUZA VIPAJI KUFANYIKA MKOANI MOROGORO


KITUO CHA UTAMADUNI NA MAENDELEO YA VIJANA TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA STUDIO YA MORO TOWN RECORD WAMEANDAA TAMASHA LA KUKUZA VIPAJI MKOANI MOROGORO.
TAMASHA HILO LINALOSHIRIKISHA VIJANA 250 KUTOKA MKOA WA MOROGORO,PWANI NA MAENEO YA HKARIBU YALIANZA JANA MJINI MOROGORO,
LENGO LA TAMASHA HILI NI KUKUZA VIPAJI.AMBAPO WASHINDI WATAPATA BAHATI YA KURECORD ALBUM MOJA MOJA NA WASHINDI KWA UPANDE WA MAIGIZO WATAPATA BAHATI YA KUREKODI FILAMU,
SHINDANO HILO  LITAKUWA LINARUSHWA MOJA KWA MOJA NA TELEVISION YA ABOOD YA MJINI MOROGORO ILI KUWAPA WATAZAMAJI FURSA YA KUWAPIGIA KURA WASHIRIKI

Washiriki wa maigizo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchujo katika tamasha hilo la kukuza vipaji mkoani morogoro

 Washiriki wa kuimba wakiwa katika picha ya pamoja

Washiriki wa shindano hilo Paulo Lucas na Denis wakiwa katika pozi kabla ya shindano hilo kuanza jana mkoani morogoro

MKUU WA WILAYA YA TANGA ATEMBELEA TIMU NZIMA YA SERENGETI FIESTA 2012

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (kushoto) akiongea machache mara baada ya kutembelea timu nzima ya Serengeti Fiesta 2012. Ambapo Mkuu huyo wa wilaya alisisitiza watu wajitokeze kwa wingi uwanja wa Mkwakwani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 huku akitoa msisitizo kwa wakazi wa Tanga kujitokeza katika zoezi la sensa. Tamasha la Serengeti Fiesta linatarajiwa kufanyika leo tarehe 26.8.2012
 Baadhi ya wageni wakimsikiliza kwa makini mkuu huyo wa wilaya ya Tanga.
Afisa Mausiano wa Clouds Media Group, Simon Simalenga akitoa msisitizo wa jambo mbele ya mkuu wa vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego.
…akiaga mara baada ya maongezi machache.

AUDITION YA ‘ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013′ IMEANZA KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR.


Pichani Juu na Chini ni Sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajli ya majaji pamoja na Jukwaa la kutembelea Models.

Majaji watakaofanya Usaili wa kutafuta wanamitindo watakaoshiriki kwenye Onyesho la Mavazi la Ally Rehmtullah Collection 2013 litakalofanyika tarehe 8 September 2012 wakibadilishana mawazo leo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar kabla ya kuanza usaili huo.

Baadhi ya Models waliojitokeza kushiriki katika usaili huo wakitafakari itakuwaje…???Kwa wanaotaka kushiriki endeleeni kujitokeza.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ASHIRIKI ZOEZI LA SENSA JIJINI DAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijiandaa kujibu maswali kutoka kwa Karani wa Sensa, Happyness Masaka (kulia) ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi hilo la Senza ya watu na Makazi, lililoanza  leo nchini kote, ambalo litadumu kwa siku saba. Picha na OMR
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Agosti 26, saa tatu asubuhi, ameshiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya watu na Makazi akiwa kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 Dkt. Bilal, ameshiriki katika zoezi hilo kwa kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Karani wa Kituo cha Oysterbay, Happyness Masaka, mbaye alifika nyumbani kwa makamu akiwa ameongozana na msimamizi wake, Daria Kailembo, pamoja na Maofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Stanley Mahembe na Radegunda Maro.
 Aidha, Dkt. Bilal, ametumia dakika 25 kwa kujibu jumla ya maswali 37, yaliyoandaliwa ili kukamilisha zoezi hilo.
 Akizungumza baada ya kukamilisha zoezi hilo, Dkt. Bilal, amewahasa Watanzania wote kwa ujumla kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha zoezi hilo, ambalo litadumu kwa siku saba.

RAIS DK SHEIN AHESABIWA KATIKA HUKO MIGOMBANI UNGUJA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Ali Moahmed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema
Shein,pamoja na familia yao walipojiandikisha  kwa katika zoezi la
Sensa ya Watu na Makaazi, lililoanza leo nchini kote, wakiwa katika
Shehia ya Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,   [Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Ali Moahmed Shein,akijiandikisha na  familia yake kwa
Karani Asia Hassan Mussa,(kushoto) katika zoezi la Sensa ya Watu na
Makaazi, lililoanza leo nchini kote,Rais  akiwa katika  Shehia ya
Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,(kulia ) Mke wa Rais Mama
Mwanamwema Shein,  [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

TAARIFA YA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilifanya kikao cha kawaida cha siku moja mjini Dar es salaam tarehe 24/08/2012 chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. 
Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imefanya yafuatayo;-
 
#. Imepokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa maagizo yake juu ya kushughulikia mapungufu yaliyoonyeshwa kwenye taarifa ya CAG na Kamati mbalimbali za bunge.
#. Imeipongeza serikali kwa hatua zilizoanza kuchukuliwa dhidi ya mapungufu hayo, hasa hatua dhidi ya wakuu mbalimbali wa mashirika kadhaa ya umma, kama vile TANESCO, TBS,  BANDARI , ATC,MALIASILI nk.
**Itakumbukwa Kamati Kuu iliagiza pamoja na viongozi wa kisiasa kuchukuliwa hatua kwa mapungufu yale, ipo haja ya kuwachukulia hatua watendaji wakuu wa mashirika yaliyohusishwa na ubadhirifu mbalimbali. 
 #. Kamati Kuu inawapongeza mawaziri husika na watendaji wote wa serikali walioanza kutekeleza agizo hili kwani mwisho wa siku maisha bora kwa kila mtanzania yatawezekana.
 #.Pamoja na pongezi hizo, Kamati Kuu imeielekeza serikali kuendelea kuchukua hatua zaidi ili kufikia lengo lililokusudiwa.
 #. Kamati Kuu ilipokea pia taarifa ya mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania kwenye ziwa Nyasa na hatua zilizochukuliwa kutatua mgogoro huo. Kamati kuu ikaazimia yafuatayo;
 (i). Imeipongeza serikali kwa hatua inazochukua za kupata suluhisho la mgogoro huo kwa njia ya amani.
(ii). Kamati Kuu inawatahadharisha wanasiasa na vyombo vya habari vinavyochochea vita na uhasama kati ya Tanzania na Malawi kuacha mara moja na kuiachia diplomasia ichukue mkondo wake.
(iii). Kamati Kuu imeitaka serikali kwakuwa tatizo hili limekuwa la muda na linajirudia mara kwa mara sasa kulishighulikia swala hili mpaka mwisho.
 #.  Kamati Kuu pia ilipokea taarifa ya maendeleo ya uchaguzi ndani ya Chama, iliridhishwa na maendeleo hayo ya uchaguzi na kuagiza yafuatayo;-
(i). Kila kikao husika kihakikishe haki inatendeka hasa katika zoezi la uchujaji wa majina.
(ii). Kuendelea kukemea vitendo vya rushwa kwenye chaguzi zetu. Na kuhakikisha kila anayebainika kujihusisha na vitendo hivyo au mawakala wao hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
(iii). Kamati Kuu imeyapongeza mashina, matawi na kata zilizokamilisha zoezi hili kwa ufanisi.

POSHO ZA WENYEVITI ZIPO PALEPALE – PINDA, AHESABIWA KIJIJINI KWAKE KIBAONI- KATAVI


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihojiwa na Karani wa sensa, Beatrice Nchimbi wakati alipojiandikisha kijini kwake Kibaoni, mkoani Katavi, Agust 26,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*Ahesabiwa kijijini kwake Kibaoni

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema posho kwa ajili ya wenyeviti wa vitongoji na vijiji ambao wataambatana na makarani wa sensa zipo palepale na kwamba hawana haja ya kuhofu juu ya malipo yao.
 Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumapili, Agosti 26, 2012) mara baada ya kuhojiwa na maafisa wa sensa kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele, mkoani Katavi.
 Waziri Mkuu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Sensa amewasihi wenyeviti hao waendelee na kazi yao bila wasiwasi wowote kwani watalipwa. “Ni kweli malipo yao yamechelewa, ni suala la wikiendi tu kuingilia hapa kati, lakini napenda niwahakikishie kwamba stahili zao zipo, wao wachape kazi tu!” alisisitiza.
 Alisema ameona kwenye taarifa za habari kupitia baadhi ya luninga wakidai kwamba wameachwa katika malipo ya kazi hiyo lakini akatumia fursa hiyo kuwahakikishia kwamba watalipwa. “Nimeona kwenye TV wanadai kuwa wameachwa, si kweli. Nawahakikishia wote kwamba wako katika hesabu yetu na wote watalipwa,” aliongeza.
 Akizungumzia kuhusu zoezi zima la sensa ya makazi na watu, Waziri Mkuu Pinda aliwaomba Watanzania watambue kuwa zoezi hili lilianza tangu mwaka 2004 na lina gharama kubwa kwani mpaka sasa limegharimu zaidi ya sh. bilioni 140/-.
 “Hili ni jambo linalopaswa kupewa nafasi kubwa na kila Mtanzania kwani lengo lake ni kuiwezesha Serikali kujua idadi ya watu tulionao, na itusaidie kupanga maendeleo yetu,” alisema.
 “Serikali inao mpango wa miaka mitano, ifikapo mwaka kesho na mwaka kesho kutwa tutaweza kujua malengo yetu na kuweka mbinu za kuitekeleza mipango yetu… ,” alisema.
 Alisema ukweli huo unabainishwa na maswali yaliyomo kwenye dodoso la sensa ambayo yanalenga kujua jinsi za watu, umri wao, shughuli zao za kiuchumi na kuwaweka katika makundi ili iwe rahisi kuwahudumia. “Tunaangalia jinsi za watu, rika zao, na hata makundi ya walemavu ili tuweze kubainisha mahitaji yao na kuwafikishia huduma kwa urahisi,” alisema.
 Aliwasihi Watanzania ambao hawatahesabiwa leo kuwa wavumilivu kwani zoezi hilo litaendelea kwa muda wa siku saba. “Makarani wataendelea kutembelea kaya kwa siku saba zijazo, cha msingi mkuu wa kaya aandae taarifa za watu waliolala kwenye mji wake usiku wa tarehe 25 kuamkia tarehe 26 Agosti, mwaka huu. Aorodheshe majina yao, umri wao, elimu yao, jinsi zao na shughuli ambazo wanazifanya,” alifafanua.
 Kuhusu watu wanaopinga sensa, Waziri Mkuu alisema anaunga mkono kauli zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein la kuwataka Watanzania wote washiriki zoezi la sensa.
 “Viongozi wetu wa kitaifa wamelielezea vizuri suala hili na hasa kuhusu kipengele cha dini. Hayo madai si zoezi lake kwa sasa,” alisema.

Neno La Maggid Mjengwa Leo: Nilishaamua, Nitabaki Kuwa Mjamaa

Ndugu zangu, 
Kwa siku mbili mfululizo nilikuwa kijijini Mahango, Kata ya Madibira, Mbarali, Mbeya. Huko niliongozana na wageni kutoka Uingereza waliokwenda kushiriki kazi ya ujenzi wa Maktaba ya Kijamii kijijini Mahango.
Uzoefu nilioupata kijijini Mahango ni elimu yenye gharama kubwa. Hakika nimejifunza mambo mengi. Kijijini Mahango niliuona kwa karibu sana umasikini wa watu wetu. Kwa mfano, kwenye moja ya kitongoji nilimshuhudia mama anayelindia maji kwenye kisima chenye chemchemi yenye kutoa maji ya kujaa bakuli moja kila baada ya robo saa.
 
Mama yule kwa kauli yake alitamka huku akiwa ameshika tama; ” Hali yetu ni mbaya sana, hapa ndoo moja kujaa inaweza kunichukua saa moja na nusu”. Wakati akitamka hayo nilimwona binti wa mama huyo asiyezidi miaka kumi akiwa amesimama akimwangalia mama yake. Niliziona pia ndoo zilizopanga foleni bila wenye nazo. Bila shaka wamekwenda kujihifadhi na jua kali la mchana, na kufanya kazi nyingine pia.
 
Hali kama hiyo niliikuta pia kijijini Mapogolo. Kwenye ofisi ya Mtendaji Kata ya Miyombweni kilipo kijiji cha Mapogolo nilifanya mazungumzo na Diwani wa Kata Bw. Lokelo pamoja na  Mtendaji wa Kata Bw. Filipo. Nao  wakawa wamekunja mikono wasijue la kufanya, maana, bajeti ya Halmashauri ya kushughulikia na tatizo la maji haitoi matumaini ya kutatua tatizo la wananchi katika muda mfupi ujao. Fedha hazitoshi.
 
Kwenye Mkutano wa hadhara kijijini Mahango, Mwenyekiti wa Kijiji  alinipa nafasi adimu ya kuzungumza machache na wananchi. Nilisimama na kuwaangalia wananchi wale walioonyesha kwenye nyuso zao, kiu ya kutaka kunisikiliza; niliwaangalia akina mama na watoto migongoni, niliwaangalia watoto wale waliokaa mbele yangu. Niliwaangalia akina baba na vijana. Kwa jinsi watu walivyoitikia wito wa kukusanyika kushiriki kazi ya ujenzi wa Maktaba, kushiriki jambo la elimu, basi, nami niliyaona matumaini kwenye kusanyiko lile.

KUNDI LA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIA NCHI NCHINI THAILAND

NA EVELYN MKOKOI
KUTOKA BANGKOK THAILAND
AFISA HABARI OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Mkutano wa Kimataifa  wa mabadiliko ya Tabia nchi umeanza Nchini Thailand mjini Bangkok kama mkutano wa maandalizi ambapo, kundi la nchi za Africa zimekutana na kujadili mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na namna ya kukabiliana na kuhimili  mabadiliko ya tabia nchi.
Kundi hilo la nchi za Afrika, Likiongonzwa na uwenyikiti toka nchini Swazland, pia unategemea kupata taarifa ya mikutano mbalimbali iliyofanyika baada ya ule uliofanyika mjini Bonn mwezi May 2012.
Suala la kuhimili mabadiliko ya tabianchi bado limejitokeza kuwa ni kipaumbele kwa nchi hizo za afrika. Tanzania ambayo ni waratibu wa masuala ya hasara na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi kwa niaba ya Afrika, iliwasilisha ripoti ya mkutano wa wataalam uliofanyika Nchini Ethopia mwezi Agosti 2012 uliohusu hatua zinazofaa kumudu hasara na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabi nchi, ambapo Sudan imegusia suala la muendelezo wa washiriki katika mikutano hii ili kuweza kupata michango mizuri ya mawazo  na kitaaluma wakati wa majadiliano katika mkutano huo kutokana na yaliyojitokeza Ethipia ambapo wataalam wengi hawakushiriki.
Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika mjini Durban mwaka 2011 ulikubaliana kuanzishwa kwa chombo cha (ADP) ambacho, kitakachosimamia majadiliano ili kupata mkataba mpya utakaohusisha nchi zote katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia  nchi.
Mkutano huu wa Bangkok ndiyo mwanzo wa mchakato wa utekelezaji wa (ADP) ambapo unatakiwa ukamilike kabla ya mwaka 2015, Mkutano huu, unategemea kusikia na kujua, chombo hicho  kitafanya nini katika malengo yake ya kuhimili na kukabilianana mabadiliko ya tabia nchi, kupunguza gesi joto, kujenga uwezo katika eneo hilo pamoja na masuala ya sayansi na teknolojia na masuala ya fedha kugharamia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi..
Wakati huohuo, Kundi la nchi za Afrika pia limegusia kuhusu, mkutano mkubwa wa masuala ya mazingira utakaohusisha mawaziri wa mazingira kutoka nchi za Afrika utakaofanyika mjini Arusha mwezi September, ambapo wataalam watapata nafasi ya kujadili nafasi ya Afrika katika suala zima la mazingira ikiwa ni pamoja na kipengele cha mabadiliko ya tabia nchi kuelekea mkutano wa dunia wa mabadiliko ya tabia nchi utakaofanyika mjini Dhoha mwezi disemba mwaka huu.

HOTUBA YA MHESHIMIWA DK JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI KUHAMASISHA SENSA YA WATU NA MAKAZI, TAREHE 25 AGOSTI, 2012


 Ndugu wananchi;
Imekuwa ni mazoea yetu kuwa Rais huzungumza na taifa kila mwisho wa mwezi.  Lakini, leo nazungumza nanyi siku saba kabla ya mwisho wa mwezi kwa sababu maalum.  Sababu yenyewe si nyingine bali ni Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika kwa siku saba kuanzia kesho Jumapili tarehe 26 Agosti, 2012. Shabaha yangu ni kutaka kuwakumbusha Watanzania wenzangu wote kuhusu wajibu wao wa kujitokeza kuhesabiwa siku hizo.  Naomba kila mmoja wetu ahakikishe kuwa anakuwepo kuhesabiwa na kujibu maswali yote yatakayoulizwa na makarani wa sensa kwa ufasaha.  
 Ndugu wananchi;
Katika historia ya nchi yetu, Sensa ya mwaka huu itakuwa ni ya tano tangu Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari, 1964 na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 1964.  Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988 na 2002.  Kumbukumbu zinaonesha kuwa kwa upande wa Tanzania Bara wakati  wa ukoloni zilifanyika Sensa mwaka 1910, 1931, 1948 na  1957.  Kwa upande wa Zanzibar wakati wa ukoloni na utawala wa Sultan kulifanyika Sensa mara moja mwaka 1958. 
 Ndugu Wananchi;
Kama ilivyokuwa kwa Sensa zilizotangulia, madhumuni makubwa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ni kujua idadi ya watu,  mahali walipo, jinsia zao, umri wao, elimu, shughuli wazifanyazo, vipato vyao, upatikanaji wa huduma mbalimbali pamoja na makazi. Taarifa hizi hutumiwa na Serikali kupanga mipango ya maendeleo, kutengeneza programu mbalimbali na kubuni miradi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.  Aidha, huisaidia Serikali kupanga na kupeleka huduma za kiuchumi na kijamii kwa wananchi kwa kuzingatia mahitaji halisi ya maeneo yao wanayoishi kwa mujibu wa idadi yao na mgawanyiko wao kijinsia, kiumri na huduma zinazohitajika.  Hivyo basi, idadi halisi isipojulikana kuna hatari ya wananchi kukosa huduma wanazohitaji kwa kiwango kinachostahili.  Vilevile, takwimu hizi hutumiwa na Serikali katika kufikia uamuzi wa kugawa majimbo ya uchaguzi na maeneo ya utawala kama vile mikoa, wilaya, kata, vijiji na vitongoji vipya.

ZIARA YA WAZIRI DKT.HUVISA KILOMBERO NA ULANGA


Wazira wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Terezya Huvisa akizungumza na Wafugaji wa kijiji cha Ihanga Wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro alipowataka Wafugaji hao kuondoa Mifugo yao na kuacha Uharibifu wa Mazigira kwenye hifadhi ya Bonde la Mto Kilombero wakati wa Ziara yake Wilaya ya Ulanga na Kilombero jana {picha na Ali Meja}

WAKULIMA HUENDA WAKAINGIA KWENYE UMASIKINI KUTOKANA NA UCHAKACHUAJI WA PEMBEJEO

 WAKULIMA nchini huenda wakaingia kwenye umasikini wakutisha kutokana na uchakachuaji wa pembejeo unaofanywa na baadhi ya wa Waingizaji na Wasambazaji wa pembejeo na dawa za mifugo hizo.
 Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki, na wadau wa usambazaji mbolea, viuatilifu na madawa ya mifugo kwa wakulima wadogo wadogo, waliyoshiriki washa ya siku moja kujadili Ripoti ya utafiti iliyofanywa na Baraza la Kilimo (ACT), hivi karibuni.
 Walisema tatizo hilo la uchakachuaji wa madawa na utengezaji wa mbolea bandia limekuwa likienea kwa kasi kubwa, karibu nchi nzima hali inayoashiria kuharibu udongo na kuua mazao yote yanayo mwagiliwa mbolea na madawa hayo.
 Mmoja wa washiriki wa washa hiyo, Suleiman Khamisi, salibainisha kuwa tatizo hilo ni kubwa na kama serikali haita kuwa makini katika kulidhibiti kuna hatari nchi hii ikaja kukumbwa na janga la njaa.
 “Viongozi wetu wanapaswa walione hili na kwa pamoja tu tuelekeze nguvu zetu kama ilivotokea kwenye vita ya uchakachuaji wa mafuta ambapo ili saidia kupunguza tatizo hilo japo kwa kiasi”alisema Khamisi.
 Alisema kutokana na wakuliama kutokuwa na utaalamu wa kutambua mbolea au dawa ipi ni badia wanalazimika kuzinunua bila kujua madhara yatakayojitokeza baadaye.
 Khamisi alisema pembejeo hizo zimekuwa zikiwatia hasara wakulima wakati wa mavuno, hivyo kuwaingiza kwenye migogoro na taasisi za fedha kutokana na kukosa fedha za kulipa mikopo waliyokopa kwa ajili ya kilimo.
 Pia vitendo hivyo vinaathili soko la nje kwa kuwakimbiza wafanyabiashara wanje kuacha kuja kununua pembejeo hizo badala yake kuhamia nchi nyingine.
 Awali Mtaalamu Mwelekezi, Edmund Ringo, alisema tatizo hilo la  uchakachuaji pembejeo na viuatilifu limejitokeza katika maeneo mbalimbali walioyafanyia utafiti, inaonyesha tatizo hilo liko karibu nchi nzima.
Alisema kuwa vitendo hivyo, vimekuwa vikifanywa na baadhi ya makundi ya watu wenye tama ambapo kukomesha hali hiyo, kunaulazima kwa Baraza hilo kutunga sera ambayo italinda maslahi.

PRO-LIFE yawataka watanzania kuwa makini na vidhibiti mimba

 SHIRIKA la Kutetea Uhai wa Binadamu nchini (PRO-LIFE), limewataka Watanzania kuwa makini katika matumizi ya dawa za vizibiti mimba,lengo lake likiwa nikupunguza idadi ya watu ili mataifa makubwa yaendelee kupora rasilimali za Waafrika.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mtafiti wa Elimu kutoka nchini Marekan, Brian Clowes, alisema Tanzania haina haja ya wananchi wake kujiingiza katika kampeni hiyo wa vidhibiti mimba, Tanzania bado inaidadi ndogo ya watu ukilinganisha na mataifa mengine duniani.
 
Alisema kampeni hiyo, lengo lake ni kuzuia ongezeko la watu, ili mataifa hayo makubwa yaweze kuendelea kuyaibia rasilimaali zao Watanzania na nchi nyingine za afrika ambapo ongezeko la watu katika nchi hizo ni kikwazo kwao.
 
“Fedha za Kampeni za uzazi wa mpango zimekuwa zikielekezwa kwenye nchi ambazo kwa kiasi kikubwa zinaongezeko la watu haswa maeneo yenye watu weusi”alisema Clowes.
 
Clowes alisema hivi sasa nchi nyingi za ulaya zimekumbwa na hofu ya kuwa na wazee wengi ukilinganisha na nchi za Afrika ambapo zinaonekana kuwa na vijana wengi.
 
Alisema mwaka 1950, Ulaya ilikuwa na asilimia 22 ya watu ambapo Bara la Afrika lilikuwa na asilimia 9 hali inayoonesha kuwa Bara hilo lilikuwa tupu.
 
Clowes alisema mwaka 1960, Bara la Ulaya lilitangaza kampeni ya kudhibiti mimba ambapo hadi mwaka 1997, idadi ya watu katika Bara hilo imezidi kupungua na inakadiriwa ifikapo mwaka 2050, litakuwa na asilimia nane ya watu huku Bara la Afrika idadi yake ya  watu ikiongezeka na kuwa asilimia 21.
 
Akizungumzia vidhibiti mimba, kingaa ya gonjwa la Ukimwi alisema siyo kweli kama kondom inauwezo wakuzuia ukimwi na mimba bali kampeni hizo zina lengo la kuvinufaisha viwanda kibiashara.
 
“Wakati zamani mataifa hayo ya Ulaya yakitumia vifaru, bastola, bunduki na ndege kuzitwala nchi hizo za kiafrika na nyingine dunia hivi sasa zimekuja na ukolino mamboleo kwa uiaminisha jamii kuwa maisha mazuri yanatokana na upangaji uzazi ambapo matumizi dawa hizo yamekuwa na athari mbaya kwa wakina mama pamoja na kuua watoto wanaotarajiwa kuzaliwa”alisema Clowes.
 
Naye Mkurugenzi wa shirika hilo, Emmil Hagamu, alisema jamii inapaswa kutumia njia za mpango wa uzazi za asili ambazo hazina madhara.
 
Alisema haamini kama matumizi ya kondom na madawa mengine kuwa ni njia salama za kudhibiti mimba na kupunguza maambukizi ya maradhi ya ukimwi.
 
Hagamu aliitaka jamii kutambua kuwa nchi nyingi zilizojiingiza kwenye matumizi ya kondom ndizo zimekuwa zikiongoza kwa maambukizi ya ukimwi kutokana na kondom nyingi kuwa hazifanyi kazi tangu zikiwa kiwandani.
 
Alitoa wito kwa kuitaka jamii kubadili mitazamo katika kujiepusha na ngono zembe kama wanavyoishi watu wenye mitazamo ya kidini kutoka Afrika ya kasikazini ambapo wanaamini ndoa ndiyo dawa ya kudhibiti maambukizi mapya ya Ukimwi.

Wenyeviti wa vitongoji 116 mkoani Kilimanjaro wafuta tishio la kutoshiriki sensa

Na.Ashura Mohamed-Hai
Wenyeviti wa vitongoji na vijiji wapatao 116 katika wilaya ya Hai wameondoa tishio lao la kutoshiriki katika sensa na kuahidi kushirikiana na makarani wa zoezi katika kuhakikisha linafanikiwa
 Wenyeviti hao walitoa tishio hilo kwa barua kwenda kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Hai na kumkabidhi nakala mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw Leonidas Gama alipokuwa katika ziara ya kuhamasisha sensa wilayani Hai Jumanne iliyopita.
 Wenyeviti hao walifuta mpango
huo baada ya kuwa na kikao cha saa mbili na mkuu wa wilaya ya Hai Bw Novatus Makunga na kuahidi kuongoza makarani wa sensa katika vitongoji vyao
 Kaimu mwenyekiti wa umoja wa wenyeviti wa vitongoji wilayani Hai Bw Simon Mnyampanda ameeleza kuwa baada ya kikao hicho na mkuu wa wilaya ya hai Bw Makunga sasa wamepata ari na nguvu ya kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa.
 Tamko hilo ambalo limesainiwa na wenyeviti wapatao 103 kwenda kwa mkuu wa wilaya na nakala kwa mkuu wa mkoa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya wameeleza kwa kauli moja wanafuta tamko la awali ambalo lilikuwa likieleza kuwa hawatajihusisha na kuwaongoza makarani kwa zoezi la sensa katika vitongoji vyao kwa kuwa hawajuhi mipaka na ukomomo wao na sheria na kanuni za sensa.
 Naye mkuu wa wilaya hiyo Bw Novatus Makunga aliwataka wenyeviti hao kabla ya kushiriki katika zoezi hilo kufuta tamko lao kwa maandishi agizoi ambalo walikubali na baadaye kukutana na kutoa waraka wa kufuta tamko la wali la tarehe 17/08/2012 la kutowaongoza makarani wa sensa
 Baada ya kukubali kuliondoa na kulifuta tamko lao,Bw Makunga aliwaagiza waratibu wa sensa wilayani humu kuwagawia nyaraka na vipeperushi mbalimbali vinavyohusu sensa na pia aliwafafanualia kuwa katika kazi hiyo tayari  ofisi ya taifa ya takwimu imetoa muongozo wa wenyeviti hao kulipwa posho maalumu ya kuwaongoza makarani
 Wenyeviti hao walitangaza kususia zoezi la sensa wakishinikiza kulipwa posho zao za jumla ya shiulingi milioni 280 wanazodai kwamba halmashauri ya wilaya hiyo haijawalipa tangu mwaka 2008
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw Leonidas Gama kutokana na barua hiyo aliwapa siku moja wenyeviti hao kuandika barua ya kujitoa katika ushiriki wa zoezi hilo endapo msimamo wao unabaki pale pale wa kutotoa  ushirikiano kwa makarani wa sensa

Rais Dk.Shein akutana na Mwakilishi wa Kudumu wa Tz katika UN


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi Tuvuko Manongi,mwakilishi
wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Nchini Marekeni,(kulia)
alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais jana na katikati
Naibu wake Balozi Ramadhan Muombwa .[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi Tuvuko
Manongi,mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Nchini Marekeni,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais
jana,(kushoto) ni Naibu wake  Balozi Ramadhan Muombwa.   .[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Balozi Tuvuko
Manongi,Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Nchini Marekeni,(kushoto)alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo
na Rais jana,katikati naibu wake  Balozi Ramadhan Muombwa.  .[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]

WAZIRI MKUU PINDA AFANYA ZIARA YA KATAVI


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Rajabu Rutengwe baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kwa ziara ya jimbo Agust 25,2012.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

WAMILIKI WA VYUO WATAKIWA KUAJIRI WALIMU WENYE SIFA ZA KUFUNDISHA

Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha

WAMILIKI wa Vyuo Binafsi kwa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatoa ajira kwa wafanyakazi wenye sifa kwani endapo kama watatoa ajira kwa watu ambao hawana sifa ni wazi kuwa watakuwa ni chanzo cha Umaskini hasa kwenye sekta ya ajira binafsi.
 Kauli hiyo imetolewa leo na Diwani wa kata ya Ngarenaro Bw Isaya Doita wakati akiongea katika maafali ya pili ya chuo cha Hoteli cha Fountain Justice Training College(FJTC) kilichopo Sakina mjini hapa
 Bw Doita alisema kuwa vyuo Binafsi vina nafasi kubwa sana ya kuweza kusaidia maendeleo ya jamii hasa pale ambapo kama watatoa ajira kwa watu wenye sifa lakini pia vyuo hivyo vina wezakuwa Chanzo cha kukosa ajira hasa pale ambapo wataajiri watu ambao hawana sifa maalumu ya kufundisha katika vyuo hivyo
 Alisema kuwa Kamwe vyuo vilivyopo katika maeneo mbalimbali ya mitaa havipaswi kuona kuwa havina mchango kwa jamii badala yake vyuo hivyo vinatakiwa kujijenga na kujiimarisha zaidi ili view ni chachu ya mafanikio hasa katika suala zima la Ajira hapa Nchini
 Alifafanua kuwa kama Vyuo vyote vitalenga kuwa na mitaala ambayo inakubalika ndani ya jamii basi mbali na kutoa ajira kwa wanafunzi ambao wanaitimu katika vyuo hivyo basi vitachangia sana wanafunzi kuweza kujiajiri wao wenyewe na kuachana na tabia ya kusubiri kuajiriwa wakati uwezo wa kujiajiri wao kama waitimu upo
 “kwa sasa vipo baadhi ya vyuo ambavyo vinaajiri hata walimu ambao hawana uwezo wakidhani kuwa hawaonekani na jamii lakini wajue kuwa wao wanachangia sana umaskini kwenye jamii yetu kwani Lengo la hivi Vyuo ni kuhakikisha kuwa vinaboresha maisha ya Watanzania kwa maana hiyo ni vizuri kama kila Mkurugenzi wa chuo akahakikisha kuwa anatoa msaada kwa jamii na wala sio kuwa chanzo cha Umaskini”aliongeza Bw Doita

LAPF YAKUTANA NA WANACHAMA WA KITUO CHA MAENDELEO YA WAHARIRI WASANIFU NA WATAYARISHAJI VIPINDI TANZANIA

Wanachama wa Kituo wamefanya kikao cha kazi pamoja na Mfuko wa LAPF leo, Agosti 25, 2012, kwenye Hoteli ya Nashera iliyopo mjini Morogoro. Lengo la kikao hicho, ambacho kilihusisha wanachama 25 wa Kituo na wataalamu wa LAPF, ilikuwa ni kuwawezesha washiriki kuelewa kazi za mfuko ili waweze kuhariri vema zaidi habari mbali mbali, hususan zile zinazohusu masuala ya mfuko huo.
Akifungua kikao hicho, Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko huo, Bw. Andrew Kuyeyana, alisisitiza umuhimu wa kutoa mafao bora zaidi kwa wanachama ili kuwawezesha kustaafu vema. Alisema Mfuko wake, ambao hadi kufikia Juni mwaka huu ulikuwa na zaidi ya wanachama 90,000, unafanya juhudi kufanikisha hilo kupitia mafao mbali mbali, ikiwa ni pamoja na pensheni, mafao kwa warithi, uzazi, gharama za mazishi, mikopo ya ujenzi wa nyumba na mikopo kwa Saccos.
Akiwasilisha mada kuhusu shughuli za Mfuko wa LAPF, Meneja za Mfuko huo kwa Kanda ya Mashariki, Bw. Sayi Lulyalya, alisema miongoni mwa mipango ya baadae ya Mfuko ni kuanzisha mafao ya elimu ili kuwapa faida zaidi wanachama.
Naye Meneja wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Elias Baruti, alisema miongoni mwa changamoto zinazoukabili Mfuko ni jinsi ya kuwezesha upatikanaji wa faida ya kuridhisha katika hali ya uchumi ambao unaathiriwa na mfumuko wa bei.
Meneja huyo alisema miongoni mwa mipango ya baadaye ya Mfuko huo ni kuwezesha ujenzi wa miji midogo (satellite towns) katika maeneo mbali mbali nchini ili kutoa nafasi za ofisi na biashara.
Akitoa neno la shukrani, Mwenyekiti wa Kituo, Lauden Mwambona, alisema wahariri wasanifu na watayarishaji vipindi wanatakiwa kuwa na uelewa mkubwa na wa kina zaidi wa masuala mbali mbali ya kitaifa na kimataifa ili waweze kuhariri habari kwa ufanisi zaidi.