UZINDUZI WA MRADI WA TOA TAARIFA UWE SALAMA BARABARANI JIJINI MWANZA
Mtendaji Mkuu naMkurugenziMtendaji
wa Benki ya Posta Tanzania (TPB)Sabasaba Moshingi,mwenye suti ,akiteta
jambo na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani ,Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa polisi (SACP)Mohamed Mpinga,kabla ya kuzindua mradi wa Toa
Taarifa Uwe Salama Barabarani
Picha na Mashaka Baltazar wa Fullshangwe. Mwanza
Kamanda Wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, SACP Mohamed Mpinga, kulia akiwa katika picha ya
pamojanaMtendaji Mkuu na Mkurugebnzi wa Benki ya Posta,Sabasaba
Moshingi,wa tatu kutoka kulia,wa pili ni Liberatus Barlow,Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza na kushoto wa kwanza, ni Kamanda wa kikosi cha
usalama barabarani Mkoa wa Mwanza, SP Nuru Selemani katika hafla ya
uzinduzi wa mradi wa Toa taarifa Uwe Salama barabarani.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama
barabarani, Kamishna Msaidizi mwandamisi wa polisi (SACP) Mohamed
Mpinga, akitoa ufafanuzi wa jambo kwa waandishi wa habari jijini Mwanza
(hawapo pichani ) kabla ya kuzindua mradi wa Toa Taarifa Uwe
Salama.Katikati ni Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, ACP Liberatus
Barlow na kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu na Sabasaba Moshingi
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ambayo imefadhili mradi huo kwa
shilingi milioni 30.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama
barabarani ,Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP ) Mohamed Mpinga wa
kwanza kulia, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza ,Kamishna Msaidizi (ACP)
Liberatus Barlow ( wa pili kutoka kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu na
Mkurugenzi wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi mwenye suti,wakiwa
wameshika bango lenye namba za kudumu za Makamanda wa vikosi vya Usalama
barabarani wa mikoa ya Kanda ya ziwa, zitakazotumika kutoa taarifa kwa
jeshi hilo ,kuhusu ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani unaofanywa
na madereva wa magari ya abiria.Katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika
kituo kikuu cha mabasi Nyegezi na kuhudhuriwa na maofisa wa jeshi la
polisi
Kamanda wa Kikosi cha usalama
barabarani, SACP Mohamed Mpinga akiwaelekeza abiria jinsi ya kutumia
namba za kamanda wa vikosi vya usalama barabara,wakati madereva
wanapokiuka kanuni na sheria za usalama barabarani wawapo safarini
.Abiria wanapaswa kutoa taarifa kupitia namba hizo za simu ambao
zitakuwa hewani kwa saa 24.Mpinga alikuwa akizindua mradi wa Toa
taarifa Uwe salama unaofadhiliwa na Benki ya posta nchini kwa shilingi
milioni 30.
Kamanda Barlow akielekeza jambo
namna ya kutumia namba za kudumu za RTO wa mikoa yan kanda ya Ziwa
zilizopo kwenye bango lililobandikwa ndai ya basi la abiria katika kituo
cha mabasi Nyegezi muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa Toa
Taarifa uwe Salama,mradi unaofadhiliwa na Benki ya Posta Tanzania kwa
ajili ya kupunguza na kutokomeza ajali za barabarani nchini.
DIWANI KWADELO, KONDOA AHAMASISHA MAENDELEO KIAINA
Wakazi wa
Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, wanakabiliwa na uhaba
wa maji safi na salama kwa zaidi ya miaka 20 sasa, kutokana na
miundombinu iliyozinduliwa mwaka 1973, na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere, wakati wa uhai wake, kufa kwa kukosa uangalizi.
Diwani
wa Kata hiyo, Omary Kariati (wapili kulia) na Msaidizi wake Bakari Ndee
wakionyesha tangi la maji lililozinduliwa na Baba wa Taifa ambalo sasa
halifanyi kazi. Diwani alionyesha tangi hilo, wakati wa harambee ya
kuchangisha fedha za kufufua mradi wa maji. Sh. milioni 4.5, zikiwemo
sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis
Kagasheki zilipatikana. Pia gunia 37 za alizeti zenye thamani ya sh.
35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe zilichangwa kwa ajili hiyo.
Kulia ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo.
Diwani wa
Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati
akiendesha trekta wakati akiwasili kwenye hafla ya kuchangisha fedha
kwa ajili ya kufufua mradi wa maji katika kata hiyo, jana. Jumla ya sh.
milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na
Utalii, Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za
alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi
zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe. Kushoto ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh
Khamis Nchallo. .
Trekta 64
za wakulima wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, ambazo wamezipata
kwa jitihada za diwani wa kata hiyo, Omary Kariati kutoka Shirika
la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT, zikiwa zimeegeshwa eneo
la mkutano ulioitishwa na diwani huyo, kwa ajili ya harambee ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji wa kata hiyo, jana.
Wakulima hao walifika na trekta hizo na kuwa mstari wa mbele kuchangia
mradi huo wa maji. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3,
alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis
Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya
sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Wananchi wa
Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, wakiwa kwenye mkutano
wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji, katika kata
hiyo, jana. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3,
alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki
zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000
kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 1012 LAFANA UWANJA WA MKWAKWANI TANGA
Mkuu
wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego pichani kati mwenye kipaza sauti
akisoma namba za washindi waliojinyakulia piki piki mbili zilizotolewa
na kampuni ya Push Mobile,wa tatu kulia ni Meneja Masoko wa kampuni ya
Push Mobile,Rugambo Rodney na mwisho kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga,na nyuma kabisa ni
Mkurugenzi wa utafiti Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Ephrahim Mafuru
wakishuhudia tukio hilo usiku huu kwenye uwanja wa Mkwakwani ambako
tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linafanyika.
Mkuu
wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji
wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga usiku huu mara baada ya
kuwataja washindi waliojishindia piki piki mara baada ya kuchezeshwa
bahati nasibu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012
likiendelea,pichani kati ni Afisa Mahusiano wa Clouds Media Group, Simon
Simalenga.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Nuru akitumbuiza jukwaani usiku huu na
shabiki wake mbele ya wakazi wa jiji la Tanga wanaondelea kutiririka
ndani ya uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012
linafanyika.
Msanii kutoka THT,ajae kwa kasi katika anga ya muziki wa bongofleva aitwaye Rachel akiimba jukwaani usik

Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Nuru akitumbuiza jukwaani usiku huu na
shabiki wake mbele ya wakazi wa jiji la Tanga wanaondelea kutiririka
ndani ya uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012
linafanyika.
Msanii kutoka THT,ajae kwa kasi katika anga ya muziki wa bongofleva aitwaye Rachel akiimba jukwaani usiku huu.
uru akiimba kwa manjonjo na shabi wake jukwaani usiku huu.
Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua ngoma
Sehemu ya umati wa wakazi wa Tanga wakifuatilia kwa makini makamuzi ya Fiesta usiku huu.<div
Mageni asaidia ujenzi kituo cha afya Hungumalwa Kwimba
Mkufunzi Emmanuel Mageni (kushoto)
akikabidhi msaada wa mifuko 10 ya saruji kuchangia ujenzi kituo cha
afya katika Kata ya Hungumalwa wilayani Kwimba, jana. Na Mpiga Picha
wetu
Na Mwandishi wetu, Kwimba
MATUMAINI ya kukamilika kwa ujenzi
wa kituo cha afya katika Kata ya Hungumalwa wilayani Kwimba, Mwanza,
yameongezeka baada ya Mkufunzi wa Chuo cha Ualimu Murutunguru wilayani
Ukerewe, Emmanuel Mageni, kuchangia mifuko 10 ya saruji.
Mageni alikabidhi mchango wake huo kwa uongozi wa kata hiyo jana, ikiwa ni miezi minne tangu alipotoa ahadi ya kusaidia ujenzi huo katika harambee iliyoongozwa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Kangoye.
Mageni, ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alitoa msaada huo baada ya kuguswa na ukubwa wa tatizo la ukosefu wa huduma za afya za kitaalamu linaowakabili wakazi wa kata hiyo kwa muda mrefu.
Akikabidhi msaada huo jana, Mageni alitumia fursa hiyo kumpongeza Diwani wa Kata ya Hungumalwa, Shija Malando, kwa kubuni na kuhamasisha ujenzi wa kituo hicho cha afya huku akimhimiza kuongeza juhudi zaidi katika kushughulikia maendeleo ya wananchi.
“Ninakupongeza (Malando) kutokana na juhudi kubwa unazofanya katika kutafuta maendeleo ya wakazi wa Kata ya Hungumalwa, matumaini yangu ni kwamba wananchi wataendelea kukuunga mkono katika jitihada za kujiletea maendeleo,” alisema Mageni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo hicho cha afya, John Nkumba, alisema ujenzi huo ulianza mwaka jana kutokana na michango mbalimbali ya wananchi, ambapo kwa sasa umefikia hatua ya linta ukiwa umekwisha kugharimu zaidi ya sh. milioni 10.
Ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kuwaondolea wakazi 14,168 matatizo ya vifo visivyo vya lazima, wajawazito kujifungulia njiani na adha ya kutembea umbali wa kilomita 40 kwenda kutafuta matibabu wilayani Misungwi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Hungumalwa, Maneno Shaban, alimshukuru Mageni kwa kutekeleza ahadi hiyo akisema ni mfano mzuri unaopaswa kuigwa na wengine katika kuchangia maendeleo ya jamii.
Aidha, alimwomba Mageni kutosita kurudi katani hapo kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya pamoja na huduma za afya zitakazokuwa zinatolewa baada ya ujenzi huo kukamilika.
Mageni alikabidhi mchango wake huo kwa uongozi wa kata hiyo jana, ikiwa ni miezi minne tangu alipotoa ahadi ya kusaidia ujenzi huo katika harambee iliyoongozwa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Kangoye.
Mageni, ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alitoa msaada huo baada ya kuguswa na ukubwa wa tatizo la ukosefu wa huduma za afya za kitaalamu linaowakabili wakazi wa kata hiyo kwa muda mrefu.
Akikabidhi msaada huo jana, Mageni alitumia fursa hiyo kumpongeza Diwani wa Kata ya Hungumalwa, Shija Malando, kwa kubuni na kuhamasisha ujenzi wa kituo hicho cha afya huku akimhimiza kuongeza juhudi zaidi katika kushughulikia maendeleo ya wananchi.
“Ninakupongeza (Malando) kutokana na juhudi kubwa unazofanya katika kutafuta maendeleo ya wakazi wa Kata ya Hungumalwa, matumaini yangu ni kwamba wananchi wataendelea kukuunga mkono katika jitihada za kujiletea maendeleo,” alisema Mageni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo hicho cha afya, John Nkumba, alisema ujenzi huo ulianza mwaka jana kutokana na michango mbalimbali ya wananchi, ambapo kwa sasa umefikia hatua ya linta ukiwa umekwisha kugharimu zaidi ya sh. milioni 10.
Ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kuwaondolea wakazi 14,168 matatizo ya vifo visivyo vya lazima, wajawazito kujifungulia njiani na adha ya kutembea umbali wa kilomita 40 kwenda kutafuta matibabu wilayani Misungwi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Hungumalwa, Maneno Shaban, alimshukuru Mageni kwa kutekeleza ahadi hiyo akisema ni mfano mzuri unaopaswa kuigwa na wengine katika kuchangia maendeleo ya jamii.
Aidha, alimwomba Mageni kutosita kurudi katani hapo kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya pamoja na huduma za afya zitakazokuwa zinatolewa baada ya ujenzi huo kukamilika.
Wateja wafurahia Smirnoff Vodka na Smirnoff Ice katika promosheni ya Mbalamwezi Beach Club
Mkurugenzi mpya wa kampuni ya bia
ya Serengeti Bwana Steve Gannon wa pili kutoka kushoto akisakata disko
ndani ya Mbalamwezi beach club wakati wa promotion ya Smirnoff vodka na
Smirnoff ice.
Mkurugenzi mtendaji mpya wa
kampuni ya bia ya Serengeti Steve Gannon akikabidhi zawadi ya T-shirt ya
Smirnoff kwa mmoja wa washindi wa zawadi zilizotoilewa na kampuni ya
bia ya Serengeti kupitia kinywaji cha Smirnoff katika promosheni hiyo ya
Smirnoff .
Meneja wa kinywaji cha Smirnoff Bi
Azda Amani katikati akikabidhi zawadi ya T-shirt kwa mwanadada
aliyejishia zawadi hiyo kwa kucheza vizuri katika promosheni hiyo ya
Smirnoff .
RAIS KIKWETE NA FAMILIA YAKE WAHESABIWA KATIKA SENSA YA WATU NA MAKAZI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
na mkewe Mama Salma Kikwete na familia yake akijibu maswali toka kwa
karani wa sensa ya wazu na makazi Bw. Clement Ngalaba leo Agosti 26,
2012wakati alipojiunga na mamilioni ya Watanzania katika zoezi hilo
lililofanyika kwa mafanikio makubwa nchi nzima.
PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
na mkewe Mama Salma Kikwete na familia yake akijibu maswali toka kwa
karani wa sensa ya wazu na makazi Bw. Clement Ngalaba leo Agosti 26,
2012wakati alipojiunga na mamilioni ya Watanzania katika zoezi hilo
lililofanyika kwa mafanikio makubwa nchi nzima.
MDAU JANE KATUTUMIA PONGEZI ZAKE
Mdau Jane akiwa amepozi katika picha, Jane anawasalimia wadau wote wa www.fullshangweblog.com
na anasema waendelee kutembelea mtandao huu kwani unafanya kazi nzuri
ya kupasha habari katika jamii yetu, lakini pia anasema anafurahishwa na
uboreshaji wa ukurasa wa fullshangweblog kwakuwa hivi sasa picha
zinaonekana kwa ukubwa mzuri na zinavutia sana tofauti na ilivyokuwa
awali.
MISS EAST AFRICA 2012 KURUSHWA “LIVE” NA M-NET AFRICA
Miss East Africa Seychelles-Annabelle Marvel Pointe (19)
Mashindano ya Miss East Africa
mwaka huu yataonyeshwa LIVE kupitia Mnet ambapo yanatarajiwa kutuizamwa
na watu wanaokadiliwa kufikia million 200 kupitia televison na kwa njia
ya internet Dunia nzima.
Aidha maandalizi ya mashindano
hayo yanaendelea kwa kasi ambapo yamepangwa kufanyika tarehe 07
December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dare s salaam,
Tanzania badala ya mwezi September kama ilivyokuwa imetangazwa awali ili
kutoa muda zaidi kwa Ncgi ambazo hazijapata wawakilishi wao kuweza
kukamilisha zoezi hilo.
Mashindano ya Miss East Africa
mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake ambapo yatashirikisha
warembo kutoka katika Nchi 16 za ukanda wa afrika mashariki.
Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa
yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika mashariki,
pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano
hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika
Tayari baadhi ya Nchi
zinazoshiriki mashindano hayo zimeshatangaza wawakilishi wake ambazo ni
Eritrea, Ethiopia, Uganda, Southern Sudan, Malawi na Seychelles. Nchi
zilizosalia zinatarajiwa kutangaza wawakilishi wao kabla ya tarehe ya
mwisho ambayo ni tarehe 28 mwezi September.
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,
Miss East Africa Uganda-Ayisha Nagudi (23)
Miss East Africa Ethiopia-Lula Teklehaimanot (19
Miss East Africa Eritrea-Rahwa Afeworki (22)
TANZANIA YAITAKA MALAWI KUSITISHA UTAFITI KATIKA ZIWA NYASA, YASISITIZA MAZUNGUMZO LICHA YA NCHI HIYO KUENDELEA NA MSIMAMO WAKE JUU YA UMILIKI WA ZIWA HILO
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania
akisalimiana na Rais Joyce Banda wa Malawi wakati walipokutana kwenye
mkutanoa wa SADC nchini Msumbiji hivi karibuni
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Lilongwe, MALAWI.
Tanzania imeitaka Malawi kusitisha
shughuli za utafiti katika eneo la ziwa Nyasa lenye mgogoro na
kusisitiza nia yake ya kuendelea kuzungumza na nchi hiyo kuhusu mgogoro
wa mpaka licha ya nchi hiyo kuendelea na msimamo wake wa kumiliki eneo
lote la ziwa hilo.
Hayo yamebainishwa katika mkutano
wa wataalam na viongozi kutoka serikali ya Malawi na Tanzania kushindwa
kufikia muafaka uliokusudiwa kuhusu eneo halali la mpaka unaotenganisha
nchi hizo.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha
kikao cha usuluhishi kilichohusisha timu za wataalam na viongozi wa
wizara husika wa nchi hizo kilichomalizika jana usiku mjini Lilongwe
Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Bernard
Membe amesema Tanzania bado inaamini katika mazungumzo ili kufikia
muafaka wa kudumu wa mgogoro huo.
Amesema kuwa pamoja na sababu
mbalimbali zilizotolewa na upande wa serikali ya Malawi juu ya umiliki
wa eneo lote la ziwa Nyasa ,msimamo wa Tanzania juu ya mpaka
unaozitenganisha nchi hizo uko wazi kwa kwa kuzingatia vielelezo vya
historia vilivyoachwa na wakoloni na sheria za kimataifa kuhusu mpaka
kuwa katikati ya ziwa hilo.
Continue reading →
Continue reading →
TAMASHA LA KUKUZA VIPAJI KUFANYIKA MKOANI MOROGORO
KITUO CHA UTAMADUNI NA MAENDELEO YA VIJANA TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA STUDIO YA MORO TOWN RECORD WAMEANDAA TAMASHA LA KUKUZA VIPAJI MKOANI MOROGORO.
TAMASHA HILO LINALOSHIRIKISHA VIJANA 250 KUTOKA MKOA WA MOROGORO,PWANI NA MAENEO YA HKARIBU YALIANZA JANA MJINI MOROGORO,
LENGO LA TAMASHA HILI NI KUKUZA VIPAJI.AMBAPO WASHINDI WATAPATA BAHATI YA KURECORD ALBUM MOJA MOJA NA WASHINDI KWA UPANDE WA MAIGIZO WATAPATA BAHATI YA KUREKODI FILAMU,
SHINDANO HILO LITAKUWA LINARUSHWA MOJA KWA MOJA NA TELEVISION YA ABOOD YA MJINI MOROGORO ILI KUWAPA WATAZAMAJI FURSA YA KUWAPIGIA KURA WASHIRIKI
Picha na mtandao wa http://audifacejackson.blogspot.com/
Washiriki wa maigizo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchujo katika tamasha hilo la kukuza vipaji mkoani morogoro
Washiriki wa kuimba wakiwa katika picha ya pamoja
Washiriki wa shindano hilo Paulo Lucas na Denis wakiwa katika pozi kabla ya shindano hilo kuanza jana mkoani morogoro
MKUU WA WILAYA YA TANGA ATEMBELEA TIMU NZIMA YA SERENGETI FIESTA 2012
Mkuu wa Wilaya ya Tanga,
Halima Dendego (kushoto) akiongea machache mara baada ya kutembelea
timu nzima ya Serengeti Fiesta 2012. Ambapo Mkuu huyo wa wilaya
alisisitiza watu wajitokeze kwa wingi uwanja wa Mkwakwani kwenye tamasha
la Serengeti Fiesta 2012 huku akitoa msisitizo kwa wakazi wa Tanga
kujitokeza katika zoezi la sensa. Tamasha la Serengeti Fiesta
linatarajiwa kufanyika leo tarehe 26.8.2012
Baadhi ya wageni wakimsikiliza kwa makini mkuu huyo wa wilaya ya Tanga.
Afisa
Mausiano wa Clouds Media Group, Simon Simalenga akitoa msisitizo wa
jambo mbele ya mkuu wa vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego.
…akiaga mara baada ya maongezi machache.
AUDITION YA ‘ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013′ IMEANZA KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR.
Pichani Juu na Chini ni Sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajli ya majaji pamoja na Jukwaa la kutembelea Models.
Majaji
watakaofanya Usaili wa kutafuta wanamitindo watakaoshiriki kwenye
Onyesho la Mavazi la Ally Rehmtullah Collection 2013 litakalofanyika
tarehe 8 September 2012 wakibadilishana mawazo leo kwenye Hoteli ya
Serena jijini Dar kabla ya kuanza usaili huo.
Baadhi
ya Models waliojitokeza kushiriki katika usaili huo wakitafakari
itakuwaje…???Kwa wanaotaka kushiriki endeleeni kujitokeza.
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ASHIRIKI ZOEZI LA SENSA JIJINI DAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijiandaa kujibu
maswali kutoka kwa Karani wa Sensa, Happyness Masaka (kulia) ikiwa ni
sehemu ya kukamilisha zoezi hilo la Senza ya watu na Makazi, lililoanza
leo nchini kote, ambalo litadumu kwa siku saba. Picha na OMR
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Agosti 26, saa
tatu asubuhi, ameshiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya watu na Makazi
akiwa kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Dkt. Bilal,
ameshiriki katika zoezi hilo kwa kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na
Karani wa Kituo cha Oysterbay, Happyness Masaka, mbaye
alifika nyumbani kwa makamu akiwa ameongozana na msimamizi wake, Daria
Kailembo, pamoja na Maofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Stanley
Mahembe na Radegunda Maro.
Aidha, Dkt. Bilal, ametumia dakika 25 kwa kujibu jumla ya maswali 37, yaliyoandaliwa ili kukamilisha zoezi hilo.
Akizungumza
baada ya kukamilisha zoezi hilo, Dkt. Bilal, amewahasa Watanzania wote
kwa ujumla kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha
zoezi hilo, ambalo litadumu kwa siku saba.
RAIS DK SHEIN AHESABIWA KATIKA HUKO MIGOMBANI UNGUJA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Ali Moahmed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema
Shein,pamoja na familia yao walipojiandikisha kwa katika zoezi la
Sensa ya Watu na Makaazi, lililoanza leo nchini kote, wakiwa katika
Shehia ya Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, [Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
la Mapinduzi Dk.Ali Moahmed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema
Shein,pamoja na familia yao walipojiandikisha kwa katika zoezi la
Sensa ya Watu na Makaazi, lililoanza leo nchini kote, wakiwa katika
Shehia ya Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, [Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Ali Moahmed Shein,akijiandikisha na familia yake kwa
Karani Asia Hassan Mussa,(kushoto) katika zoezi la Sensa ya Watu na
Makaazi, lililoanza leo nchini kote,Rais akiwa katika Shehia ya
Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,(kulia ) Mke wa Rais Mama
Mwanamwema Shein, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
la Mapinduzi Dk.Ali Moahmed Shein,akijiandikisha na familia yake kwa
Karani Asia Hassan Mussa,(kushoto) katika zoezi la Sensa ya Watu na
Makaazi, lililoanza leo nchini kote,Rais akiwa katika Shehia ya
Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,(kulia ) Mke wa Rais Mama
Mwanamwema Shein, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TAARIFA YA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM
Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imefanya yafuatayo;-
#. Imepokea taarifa ya maendeleo
ya utekelezaji wa maagizo yake juu ya kushughulikia mapungufu
yaliyoonyeshwa kwenye taarifa ya CAG na Kamati mbalimbali za bunge.
#. Imeipongeza serikali kwa
hatua zilizoanza kuchukuliwa dhidi ya mapungufu hayo, hasa hatua dhidi
ya wakuu mbalimbali wa mashirika kadhaa ya umma, kama vile TANESCO, TBS,
BANDARI , ATC,MALIASILI nk.
**Itakumbukwa Kamati Kuu
iliagiza pamoja na viongozi wa kisiasa kuchukuliwa hatua kwa mapungufu
yale, ipo haja ya kuwachukulia hatua watendaji wakuu wa mashirika
yaliyohusishwa na ubadhirifu mbalimbali.
#. Kamati Kuu inawapongeza
mawaziri husika na watendaji wote wa serikali walioanza kutekeleza agizo
hili kwani mwisho wa siku maisha bora kwa kila mtanzania yatawezekana.
#.Pamoja na pongezi hizo, Kamati Kuu imeielekeza serikali kuendelea kuchukua hatua zaidi ili kufikia lengo lililokusudiwa.
#. Kamati Kuu ilipokea pia
taarifa ya mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania kwenye ziwa Nyasa
na hatua zilizochukuliwa kutatua mgogoro huo. Kamati kuu ikaazimia
yafuatayo;
(i). Imeipongeza serikali kwa hatua inazochukua za kupata suluhisho la mgogoro huo kwa njia ya amani.
(ii). Kamati Kuu
inawatahadharisha wanasiasa na vyombo vya habari vinavyochochea vita na
uhasama kati ya Tanzania na Malawi kuacha mara moja na kuiachia
diplomasia ichukue mkondo wake.
(iii). Kamati Kuu imeitaka
serikali kwakuwa tatizo hili limekuwa la muda na linajirudia mara kwa
mara sasa kulishighulikia swala hili mpaka mwisho.
#. Kamati Kuu pia ilipokea
taarifa ya maendeleo ya uchaguzi ndani ya Chama, iliridhishwa na
maendeleo hayo ya uchaguzi na kuagiza yafuatayo;-
(i). Kila kikao husika kihakikishe haki inatendeka hasa katika zoezi la uchujaji wa majina.
(ii). Kuendelea kukemea vitendo
vya rushwa kwenye chaguzi zetu. Na kuhakikisha kila anayebainika
kujihusisha na vitendo hivyo au mawakala wao hatua kali za kisheria
zitachukuliwa.
(iii). Kamati Kuu imeyapongeza mashina, matawi na kata zilizokamilisha zoezi hili kwa ufanisi.
POSHO ZA WENYEVITI ZIPO PALEPALE – PINDA, AHESABIWA KIJIJINI KWAKE KIBAONI- KATAVI
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akihojiwa na Karani wa sensa, Beatrice Nchimbi wakati alipojiandikisha
kijini kwake Kibaoni, mkoani Katavi, Agust 26,2012.(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
*Ahesabiwa kijijini kwake Kibaoni
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema
posho kwa ajili ya wenyeviti wa vitongoji na vijiji ambao wataambatana
na makarani wa sensa zipo palepale na kwamba hawana haja ya kuhofu juu
ya malipo yao.
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi
(Jumapili, Agosti 26, 2012) mara baada ya kuhojiwa na maafisa wa sensa
kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele, mkoani Katavi.
Waziri Mkuu ambaye ni Mwenyekiti
wa Kamati ya Kitaifa ya Sensa amewasihi wenyeviti hao waendelee na kazi
yao bila wasiwasi wowote kwani watalipwa. “Ni kweli malipo yao
yamechelewa, ni suala la wikiendi tu kuingilia hapa kati, lakini napenda
niwahakikishie kwamba stahili zao zipo, wao wachape kazi tu!”
alisisitiza.
Alisema ameona kwenye taarifa za
habari kupitia baadhi ya luninga wakidai kwamba wameachwa katika malipo
ya kazi hiyo lakini akatumia fursa hiyo kuwahakikishia kwamba watalipwa.
“Nimeona kwenye TV wanadai kuwa wameachwa, si kweli. Nawahakikishia
wote kwamba wako katika hesabu yetu na wote watalipwa,” aliongeza.
Akizungumzia kuhusu zoezi zima la
sensa ya makazi na watu, Waziri Mkuu Pinda aliwaomba Watanzania
watambue kuwa zoezi hili lilianza tangu mwaka 2004 na lina gharama kubwa
kwani mpaka sasa limegharimu zaidi ya sh. bilioni 140/-.
“Hili ni jambo linalopaswa kupewa
nafasi kubwa na kila Mtanzania kwani lengo lake ni kuiwezesha Serikali
kujua idadi ya watu tulionao, na itusaidie kupanga maendeleo yetu,”
alisema.
“Serikali inao mpango wa miaka
mitano, ifikapo mwaka kesho na mwaka kesho kutwa tutaweza kujua malengo
yetu na kuweka mbinu za kuitekeleza mipango yetu… ,” alisema.
Alisema ukweli huo unabainishwa
na maswali yaliyomo kwenye dodoso la sensa ambayo yanalenga kujua jinsi
za watu, umri wao, shughuli zao za kiuchumi na kuwaweka katika makundi
ili iwe rahisi kuwahudumia. “Tunaangalia jinsi za watu, rika zao, na
hata makundi ya walemavu ili tuweze kubainisha mahitaji yao na
kuwafikishia huduma kwa urahisi,” alisema.
Aliwasihi Watanzania ambao
hawatahesabiwa leo kuwa wavumilivu kwani zoezi hilo litaendelea kwa muda
wa siku saba. “Makarani wataendelea kutembelea kaya kwa siku saba
zijazo, cha msingi mkuu wa kaya aandae taarifa za watu waliolala kwenye
mji wake usiku wa tarehe 25 kuamkia tarehe 26 Agosti, mwaka huu.
Aorodheshe majina yao, umri wao, elimu yao, jinsi zao na shughuli ambazo
wanazifanya,” alifafanua.
Kuhusu watu wanaopinga sensa,
Waziri Mkuu alisema anaunga mkono kauli zilizotolewa na Rais Jakaya
Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein la kuwataka
Watanzania wote washiriki zoezi la sensa.
“Viongozi wetu wa kitaifa
wamelielezea vizuri suala hili na hasa kuhusu kipengele cha dini. Hayo
madai si zoezi lake kwa sasa,” alisema.
Neno La Maggid Mjengwa Leo: Nilishaamua, Nitabaki Kuwa Mjamaa
Ndugu zangu,
Kwa siku mbili mfululizo
nilikuwa kijijini Mahango, Kata ya Madibira, Mbarali, Mbeya. Huko
niliongozana na wageni kutoka Uingereza waliokwenda kushiriki kazi ya
ujenzi wa Maktaba ya Kijamii kijijini Mahango.
Uzoefu nilioupata kijijini
Mahango ni elimu yenye gharama kubwa. Hakika nimejifunza mambo mengi.
Kijijini Mahango niliuona kwa karibu sana umasikini wa watu wetu. Kwa
mfano, kwenye moja ya kitongoji nilimshuhudia mama anayelindia maji
kwenye kisima chenye chemchemi yenye kutoa maji ya kujaa bakuli moja
kila baada ya robo saa.
Mama yule kwa kauli yake
alitamka huku akiwa ameshika tama; ” Hali yetu ni mbaya sana, hapa ndoo
moja kujaa inaweza kunichukua saa moja na nusu”. Wakati akitamka hayo
nilimwona binti wa mama huyo asiyezidi miaka kumi akiwa amesimama
akimwangalia mama yake. Niliziona pia ndoo zilizopanga foleni bila wenye
nazo. Bila shaka wamekwenda kujihifadhi na jua kali la mchana, na
kufanya kazi nyingine pia.
Hali kama hiyo niliikuta pia
kijijini Mapogolo. Kwenye ofisi ya Mtendaji Kata ya Miyombweni kilipo
kijiji cha Mapogolo nilifanya mazungumzo na Diwani wa Kata Bw. Lokelo
pamoja na Mtendaji wa Kata Bw. Filipo. Nao wakawa wamekunja mikono
wasijue la kufanya, maana, bajeti ya Halmashauri ya kushughulikia na
tatizo la maji haitoi matumaini ya kutatua tatizo la wananchi katika
muda mfupi ujao. Fedha hazitoshi.
Kwenye Mkutano wa hadhara
kijijini Mahango, Mwenyekiti wa Kijiji alinipa nafasi adimu ya
kuzungumza machache na wananchi. Nilisimama na kuwaangalia wananchi wale
walioonyesha kwenye nyuso zao, kiu ya kutaka kunisikiliza;
niliwaangalia akina mama na watoto migongoni, niliwaangalia watoto wale
waliokaa mbele yangu. Niliwaangalia akina baba na vijana. Kwa jinsi watu
walivyoitikia wito wa kukusanyika kushiriki kazi ya ujenzi wa Maktaba,
kushiriki jambo la elimu, basi, nami niliyaona matumaini kwenye
kusanyiko lile.
KUNDI LA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIA NCHI NCHINI THAILAND
KUTOKA BANGKOK THAILAND
AFISA HABARI OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Mkutano wa Kimataifa wa
mabadiliko ya Tabia nchi umeanza Nchini Thailand mjini Bangkok kama
mkutano wa maandalizi ambapo, kundi la nchi za Africa zimekutana na
kujadili mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na namna ya kukabiliana na
kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Kundi hilo la nchi za Afrika,
Likiongonzwa na uwenyikiti toka nchini Swazland, pia unategemea kupata
taarifa ya mikutano mbalimbali iliyofanyika baada ya ule uliofanyika
mjini Bonn mwezi May 2012.
Suala la kuhimili mabadiliko ya
tabianchi bado limejitokeza kuwa ni kipaumbele kwa nchi hizo za afrika.
Tanzania ambayo ni waratibu wa masuala ya hasara na madhara yatokanayo
na mabadiliko ya tabia nchi kwa niaba ya Afrika, iliwasilisha ripoti ya
mkutano wa wataalam uliofanyika Nchini Ethopia mwezi Agosti 2012
uliohusu hatua zinazofaa kumudu hasara na madhara yatokanayo na
mabadiliko ya tabi nchi, ambapo Sudan imegusia suala la muendelezo wa
washiriki katika mikutano hii ili kuweza kupata michango mizuri ya
mawazo na kitaaluma wakati wa majadiliano katika mkutano huo kutokana
na yaliyojitokeza Ethipia ambapo wataalam wengi hawakushiriki.
Mkutano wa mabadiliko ya tabia
nchi uliofanyika mjini Durban mwaka 2011 ulikubaliana kuanzishwa kwa
chombo cha (ADP) ambacho, kitakachosimamia majadiliano ili kupata
mkataba mpya utakaohusisha nchi zote katika kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi.
Mkutano huu wa Bangkok ndiyo
mwanzo wa mchakato wa utekelezaji wa (ADP) ambapo unatakiwa ukamilike
kabla ya mwaka 2015, Mkutano huu, unategemea kusikia na kujua, chombo
hicho kitafanya nini katika malengo yake ya kuhimili na kukabilianana
mabadiliko ya tabia nchi, kupunguza gesi joto, kujenga uwezo katika eneo
hilo pamoja na masuala ya sayansi na teknolojia na masuala ya fedha
kugharamia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi..
Wakati huohuo, Kundi la nchi za
Afrika pia limegusia kuhusu, mkutano mkubwa wa masuala ya mazingira
utakaohusisha mawaziri wa mazingira kutoka nchi za Afrika utakaofanyika
mjini Arusha mwezi September, ambapo wataalam watapata nafasi ya
kujadili nafasi ya Afrika katika suala zima la mazingira ikiwa ni pamoja
na kipengele cha mabadiliko ya tabia nchi kuelekea mkutano wa dunia wa
mabadiliko ya tabia nchi utakaofanyika mjini Dhoha mwezi disemba mwaka
huu.
HOTUBA YA MHESHIMIWA DK JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI KUHAMASISHA SENSA YA WATU NA MAKAZI, TAREHE 25 AGOSTI, 2012
Ndugu wananchi;
Imekuwa ni mazoea yetu kuwa Rais
huzungumza na taifa kila mwisho wa mwezi. Lakini, leo nazungumza nanyi
siku saba kabla ya mwisho wa mwezi kwa sababu maalum. Sababu yenyewe si
nyingine bali ni Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika kwa siku saba
kuanzia kesho Jumapili tarehe 26 Agosti, 2012. Shabaha yangu ni kutaka
kuwakumbusha Watanzania wenzangu wote kuhusu wajibu wao wa kujitokeza
kuhesabiwa siku hizo. Naomba kila mmoja wetu ahakikishe kuwa anakuwepo
kuhesabiwa na kujibu maswali yote yatakayoulizwa na makarani wa sensa
kwa ufasaha.
Ndugu wananchi;
Katika historia ya nchi yetu,
Sensa ya mwaka huu itakuwa ni ya tano tangu Uhuru wa Tanganyika mwaka
1961, Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari, 1964 na kuzaliwa kwa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 1964. Sensa nyingine
zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988 na 2002. Kumbukumbu zinaonesha kuwa
kwa upande wa Tanzania Bara wakati wa ukoloni zilifanyika Sensa mwaka
1910, 1931, 1948 na 1957. Kwa upande wa Zanzibar wakati wa ukoloni na
utawala wa Sultan kulifanyika Sensa mara moja mwaka 1958.
Ndugu Wananchi;
Kama ilivyokuwa kwa Sensa
zilizotangulia, madhumuni makubwa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka
2012 ni kujua idadi ya watu, mahali walipo, jinsia zao, umri wao,
elimu, shughuli wazifanyazo, vipato vyao, upatikanaji wa huduma
mbalimbali pamoja na makazi. Taarifa hizi hutumiwa na Serikali kupanga
mipango ya maendeleo, kutengeneza programu mbalimbali na kubuni miradi
ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Aidha, huisaidia Serikali
kupanga na kupeleka huduma za kiuchumi na kijamii kwa wananchi kwa
kuzingatia mahitaji halisi ya maeneo yao wanayoishi kwa mujibu wa idadi
yao na mgawanyiko wao kijinsia, kiumri na huduma zinazohitajika. Hivyo
basi, idadi halisi isipojulikana kuna hatari ya wananchi kukosa huduma
wanazohitaji kwa kiwango kinachostahili. Vilevile, takwimu hizi
hutumiwa na Serikali katika kufikia uamuzi wa kugawa majimbo ya uchaguzi
na maeneo ya utawala kama vile mikoa, wilaya, kata, vijiji na vitongoji
vipya.
ZIARA YA WAZIRI DKT.HUVISA KILOMBERO NA ULANGA
Wazira wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Dk Terezya Huvisa akizungumza na Wafugaji wa kijiji cha Ihanga
Wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro alipowataka Wafugaji hao kuondoa
Mifugo yao na kuacha Uharibifu wa Mazigira kwenye hifadhi ya Bonde la
Mto Kilombero wakati wa Ziara yake Wilaya ya Ulanga na Kilombero jana {picha na Ali Meja}
WAKULIMA HUENDA WAKAINGIA KWENYE UMASIKINI KUTOKANA NA UCHAKACHUAJI WA PEMBEJEO
WAKULIMA nchini huenda
wakaingia kwenye umasikini wakutisha kutokana na uchakachuaji wa
pembejeo unaofanywa na baadhi ya wa Waingizaji na Wasambazaji wa
pembejeo na dawa za mifugo hizo.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki, na wadau wa usambazaji mbolea, viuatilifu na madawa ya mifugo kwa
wakulima wadogo wadogo, waliyoshiriki washa ya siku moja kujadili
Ripoti ya utafiti iliyofanywa na Baraza la Kilimo (ACT), hivi karibuni.
Walisema tatizo hilo la
uchakachuaji wa madawa na utengezaji wa mbolea bandia limekuwa likienea
kwa kasi kubwa, karibu nchi nzima hali inayoashiria kuharibu udongo na
kuua mazao yote yanayo mwagiliwa mbolea na madawa hayo.
Mmoja wa washiriki wa washa
hiyo, Suleiman Khamisi, salibainisha kuwa tatizo hilo ni kubwa na kama
serikali haita kuwa makini katika kulidhibiti kuna hatari nchi hii ikaja
kukumbwa na janga la njaa.
“Viongozi wetu wanapaswa
walione hili na kwa pamoja tu tuelekeze nguvu zetu kama ilivotokea
kwenye vita ya uchakachuaji wa mafuta ambapo ili saidia kupunguza tatizo
hilo japo kwa kiasi”alisema Khamisi.
Alisema kutokana na wakuliama
kutokuwa na utaalamu wa kutambua mbolea au dawa ipi ni badia
wanalazimika kuzinunua bila kujua madhara yatakayojitokeza baadaye.
Khamisi alisema pembejeo hizo
zimekuwa zikiwatia hasara wakulima wakati wa mavuno, hivyo kuwaingiza
kwenye migogoro na taasisi za fedha kutokana na kukosa fedha za kulipa
mikopo waliyokopa kwa ajili ya kilimo.
Pia vitendo hivyo vinaathili
soko la nje kwa kuwakimbiza wafanyabiashara wanje kuacha kuja kununua
pembejeo hizo badala yake kuhamia nchi nyingine.
Awali Mtaalamu Mwelekezi,
Edmund Ringo, alisema tatizo hilo la uchakachuaji pembejeo na
viuatilifu limejitokeza katika maeneo mbalimbali walioyafanyia utafiti,
inaonyesha tatizo hilo liko karibu nchi nzima.
Alisema kuwa vitendo hivyo,
vimekuwa vikifanywa na baadhi ya makundi ya watu wenye tama ambapo
kukomesha hali hiyo, kunaulazima kwa Baraza hilo kutunga sera ambayo
italinda maslahi.
PRO-LIFE yawataka watanzania kuwa makini na vidhibiti mimba
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Mtafiti wa Elimu kutoka nchini
Marekan, Brian Clowes, alisema Tanzania haina haja ya wananchi wake
kujiingiza katika kampeni hiyo wa vidhibiti mimba, Tanzania bado
inaidadi ndogo ya watu ukilinganisha na mataifa mengine duniani.
Alisema kampeni hiyo, lengo lake
ni kuzuia ongezeko la watu, ili mataifa hayo makubwa yaweze kuendelea
kuyaibia rasilimaali zao Watanzania na nchi nyingine za afrika ambapo
ongezeko la watu katika nchi hizo ni kikwazo kwao.
“Fedha za Kampeni za uzazi wa
mpango zimekuwa zikielekezwa kwenye nchi ambazo kwa kiasi kikubwa
zinaongezeko la watu haswa maeneo yenye watu weusi”alisema Clowes.
Clowes alisema hivi sasa nchi
nyingi za ulaya zimekumbwa na hofu ya kuwa na wazee wengi ukilinganisha
na nchi za Afrika ambapo zinaonekana kuwa na vijana wengi.
Alisema mwaka 1950, Ulaya
ilikuwa na asilimia 22 ya watu ambapo Bara la Afrika lilikuwa na
asilimia 9 hali inayoonesha kuwa Bara hilo lilikuwa tupu.
Clowes alisema mwaka 1960, Bara
la Ulaya lilitangaza kampeni ya kudhibiti mimba ambapo hadi mwaka 1997,
idadi ya watu katika Bara hilo imezidi kupungua na inakadiriwa ifikapo
mwaka 2050, litakuwa na asilimia nane ya watu huku Bara la Afrika idadi
yake ya watu ikiongezeka na kuwa asilimia 21.
Akizungumzia vidhibiti mimba,
kingaa ya gonjwa la Ukimwi alisema siyo kweli kama kondom inauwezo
wakuzuia ukimwi na mimba bali kampeni hizo zina lengo la kuvinufaisha
viwanda kibiashara.
“Wakati zamani mataifa hayo ya
Ulaya yakitumia vifaru, bastola, bunduki na ndege kuzitwala nchi hizo za
kiafrika na nyingine dunia hivi sasa zimekuja na ukolino mamboleo kwa
uiaminisha jamii kuwa maisha mazuri yanatokana na upangaji uzazi ambapo
matumizi dawa hizo yamekuwa na athari mbaya kwa wakina mama pamoja na
kuua watoto wanaotarajiwa kuzaliwa”alisema Clowes.
Naye Mkurugenzi wa shirika hilo,
Emmil Hagamu, alisema jamii inapaswa kutumia njia za mpango wa uzazi za
asili ambazo hazina madhara.
Alisema haamini kama matumizi ya
kondom na madawa mengine kuwa ni njia salama za kudhibiti mimba na
kupunguza maambukizi ya maradhi ya ukimwi.
Hagamu aliitaka jamii kutambua
kuwa nchi nyingi zilizojiingiza kwenye matumizi ya kondom ndizo zimekuwa
zikiongoza kwa maambukizi ya ukimwi kutokana na kondom nyingi kuwa
hazifanyi kazi tangu zikiwa kiwandani.
Alitoa wito kwa kuitaka jamii
kubadili mitazamo katika kujiepusha na ngono zembe kama wanavyoishi watu
wenye mitazamo ya kidini kutoka Afrika ya kasikazini ambapo wanaamini
ndoa ndiyo dawa ya kudhibiti maambukizi mapya ya Ukimwi.
Wenyeviti wa vitongoji 116 mkoani Kilimanjaro wafuta tishio la kutoshiriki sensa
Na.Ashura Mohamed-Hai
Wenyeviti wa vitongoji na vijiji wapatao 116 katika wilaya ya
Hai wameondoa tishio lao la kutoshiriki katika sensa na kuahidi
kushirikiana na makarani wa zoezi katika kuhakikisha linafanikiwaWenyeviti hao walitoa tishio hilo kwa barua kwenda kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Hai na kumkabidhi nakala mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw Leonidas Gama alipokuwa katika ziara ya kuhamasisha sensa wilayani Hai Jumanne iliyopita.
Wenyeviti hao walifuta mpango
huo baada ya kuwa na kikao cha saa
mbili na mkuu wa wilaya ya Hai Bw Novatus Makunga na kuahidi kuongoza
makarani wa sensa katika vitongoji vyao
Kaimu mwenyekiti wa umoja wa wenyeviti wa vitongoji wilayani
Hai Bw Simon Mnyampanda ameeleza kuwa baada ya kikao hicho na mkuu wa
wilaya ya hai Bw Makunga sasa wamepata ari na nguvu ya kushiriki
kikamilifu katika zoezi la sensa.Tamko hilo ambalo limesainiwa na wenyeviti wapatao 103 kwenda kwa mkuu wa wilaya na nakala kwa mkuu wa mkoa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya wameeleza kwa kauli moja wanafuta tamko la awali ambalo lilikuwa likieleza kuwa hawatajihusisha na kuwaongoza makarani kwa zoezi la sensa katika vitongoji vyao kwa kuwa hawajuhi mipaka na ukomomo wao na sheria na kanuni za sensa.
Naye mkuu wa wilaya hiyo Bw Novatus Makunga aliwataka wenyeviti hao kabla ya kushiriki katika zoezi hilo kufuta tamko lao kwa maandishi agizoi ambalo walikubali na baadaye kukutana na kutoa waraka wa kufuta tamko la wali la tarehe 17/08/2012 la kutowaongoza makarani wa sensa
Baada ya kukubali kuliondoa na kulifuta tamko lao,Bw Makunga aliwaagiza waratibu wa sensa wilayani humu kuwagawia nyaraka na vipeperushi mbalimbali vinavyohusu sensa na pia aliwafafanualia kuwa katika kazi hiyo tayari ofisi ya taifa ya takwimu imetoa muongozo wa wenyeviti hao kulipwa posho maalumu ya kuwaongoza makarani
Wenyeviti hao walitangaza kususia zoezi la sensa wakishinikiza kulipwa posho zao za jumla ya shiulingi milioni 280 wanazodai kwamba halmashauri ya wilaya hiyo haijawalipa tangu mwaka 2008
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw Leonidas Gama kutokana na barua hiyo aliwapa siku moja wenyeviti hao kuandika barua ya kujitoa katika ushiriki wa zoezi hilo endapo msimamo wao unabaki pale pale wa kutotoa ushirikiano kwa makarani wa sensa
Rais Dk.Shein akutana na Mwakilishi wa Kudumu wa Tz katika UN
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi Tuvuko Manongi,mwakilishi
wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Nchini Marekeni,(kulia)
alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais jana na katikati
Naibu wake Balozi Ramadhan Muombwa .[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi Tuvuko Manongi,mwakilishi
wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Nchini Marekeni,(kulia)
alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais jana na katikati
Naibu wake Balozi Ramadhan Muombwa .[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi Tuvuko
Manongi,mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Nchini Marekeni,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais
jana,(kushoto) ni Naibu wake Balozi Ramadhan Muombwa. .[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi Tuvuko
Manongi,mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Nchini Marekeni,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais
jana,(kushoto) ni Naibu wake Balozi Ramadhan Muombwa. .[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Balozi Tuvuko
Manongi,Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Nchini Marekeni,(kushoto)alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo
na Rais jana,katikati naibu wake Balozi Ramadhan Muombwa. .[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Balozi Tuvuko
Manongi,Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Nchini Marekeni,(kushoto)alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo
na Rais jana,katikati naibu wake Balozi Ramadhan Muombwa. .[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
WAMILIKI WA VYUO WATAKIWA KUAJIRI WALIMU WENYE SIFA ZA KUFUNDISHA
WAMILIKI wa Vyuo Binafsi kwa Mkoa
wa Arusha wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatoa ajira kwa wafanyakazi
wenye sifa kwani endapo kama watatoa ajira kwa watu ambao hawana sifa ni
wazi kuwa watakuwa ni chanzo cha Umaskini hasa kwenye sekta ya ajira
binafsi.
Kauli hiyo imetolewa leo
na Diwani wa kata ya Ngarenaro Bw Isaya Doita wakati akiongea katika
maafali ya pili ya chuo cha Hoteli cha Fountain Justice Training
College(FJTC) kilichopo Sakina mjini hapa
Bw Doita alisema kuwa vyuo
Binafsi vina nafasi kubwa sana ya kuweza kusaidia maendeleo ya jamii
hasa pale ambapo kama watatoa ajira kwa watu wenye sifa lakini pia vyuo
hivyo vina wezakuwa Chanzo cha kukosa ajira hasa pale ambapo wataajiri
watu ambao hawana sifa maalumu ya kufundisha katika vyuo hivyo
Alisema kuwa Kamwe vyuo vilivyopo
katika maeneo mbalimbali ya mitaa havipaswi kuona kuwa havina mchango
kwa jamii badala yake vyuo hivyo vinatakiwa kujijenga na kujiimarisha
zaidi ili view ni chachu ya mafanikio hasa katika suala zima la Ajira
hapa Nchini
Alifafanua kuwa kama Vyuo vyote
vitalenga kuwa na mitaala ambayo inakubalika ndani ya jamii basi mbali
na kutoa ajira kwa wanafunzi ambao wanaitimu katika vyuo hivyo basi
vitachangia sana wanafunzi kuweza kujiajiri wao wenyewe na kuachana na
tabia ya kusubiri kuajiriwa wakati uwezo wa kujiajiri wao kama waitimu
upo
“kwa sasa vipo baadhi ya vyuo
ambavyo vinaajiri hata walimu ambao hawana uwezo wakidhani kuwa
hawaonekani na jamii lakini wajue kuwa wao wanachangia sana umaskini
kwenye jamii yetu kwani Lengo la hivi Vyuo ni kuhakikisha kuwa
vinaboresha maisha ya Watanzania kwa maana hiyo ni vizuri kama kila
Mkurugenzi wa chuo akahakikisha kuwa anatoa msaada kwa jamii na wala sio
kuwa chanzo cha Umaskini”aliongeza Bw Doita
LAPF YAKUTANA NA WANACHAMA WA KITUO CHA MAENDELEO YA WAHARIRI WASANIFU NA WATAYARISHAJI VIPINDI TANZANIA
Akifungua kikao hicho, Meneja
Masoko na Uhusiano wa Mfuko huo, Bw. Andrew Kuyeyana, alisisitiza
umuhimu wa kutoa mafao bora zaidi kwa wanachama ili kuwawezesha kustaafu
vema. Alisema Mfuko wake, ambao hadi kufikia Juni mwaka huu ulikuwa na
zaidi ya wanachama 90,000, unafanya juhudi kufanikisha hilo kupitia
mafao mbali mbali, ikiwa ni pamoja na pensheni, mafao kwa warithi,
uzazi, gharama za mazishi, mikopo ya ujenzi wa nyumba na mikopo kwa
Saccos.
Akiwasilisha mada kuhusu shughuli
za Mfuko wa LAPF, Meneja za Mfuko huo kwa Kanda ya Mashariki, Bw. Sayi
Lulyalya, alisema miongoni mwa mipango ya baadae ya Mfuko ni kuanzisha
mafao ya elimu ili kuwapa faida zaidi wanachama.
Naye Meneja wa Mipango na
Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Elias Baruti, alisema miongoni mwa
changamoto zinazoukabili Mfuko ni jinsi ya kuwezesha upatikanaji wa
faida ya kuridhisha katika hali ya uchumi ambao unaathiriwa na mfumuko
wa bei.
Meneja huyo alisema miongoni mwa
mipango ya baadaye ya Mfuko huo ni kuwezesha ujenzi wa miji midogo
(satellite towns) katika maeneo mbali mbali nchini ili kutoa nafasi za
ofisi na biashara.
Akitoa neno la shukrani,
Mwenyekiti wa Kituo, Lauden Mwambona, alisema wahariri wasanifu na
watayarishaji vipindi wanatakiwa kuwa na uelewa mkubwa na wa kina zaidi
wa masuala mbali mbali ya kitaifa na kimataifa ili waweze kuhariri
habari kwa ufanisi zaidi.
RECENT COMMENTS