Serikali yaomba baraka za Mchungaji Loliondo | Send to a friend |
Thursday, 24 March 2011 21:36 |
0diggsdigg KIKAO cha kutafuta njia bora ya kuwawezesha wananchi kupata tiba ya magonjwa sugu huko Loliondo kilichoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na viongozi wa mikoa sita wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdore Shirima na mwenzake wa Mara, Enos Mfuru kimeahirishwa katika kile kinachoaminika kuwa ni hadi pale maazimio yake yatakapopata baraka za Mchungaji Ambilikile Mwasapile. Lukuvi aliwaambia waandishi wa habari mara baada ya kuahirisha kikao hicho saa 3:35 usiku kuwa bado kuna mambo ya kujadiliwa kabla ya kutoa tamko rasmi.“Kikao kimeahirishwa tumepeana majukumu, kesho Mkuu wa Mkoa wa Arusha atakuwa Loliondo kuongea na Mchungaji Ambilikile Mwasapile na kujionea hali ilivyo kwa sasa na wengine wamepewa majukumu mengine, hivyo kesho (leo) tutakuwa na la kuwaambia baada ya RC kurudi," alisema. Kwa muda wa siku nzima viongozi hao walikuwa katika Ukumbi wa Ofisi namba 40 katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha, wakijadili hali ilivyo huko Loliondo hasa baada ya mvua kuanza kunyesha na kusababisha msongamano mkubwa magari. Mbali ya viongozi hao, mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Serikali kutoka Mikoa ya Singida, Kilimanjaro, Manyara na Shinyanga, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga na vingozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati. Habari zilizopatikana baada ya kikao hizo zinasema Serikali inakusudia kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, mahema ya kutosha ambayo yatakodishwa kwa wananchi wanaokwenda huko. Pia Serikali imerejea ahadi iliyoitoa wiki kadhaa zilizopita ya kuandaa utaratibu wa kuwasaidia wagonjwa waliozidiwa kupata huduma haraka kwa kutumia gari la kubebea wagonjwa (ambulance) ambalo kwa sasa limeshindwa kufanya hivyo kutokana na baadhi ya watu kudai gari hilo linatumika kuwabeba vigogo badala ya wagonjwa wenye hali mbaya. Taasisi yajitokeza kujenga vyoo, mahema Taasisi ya kimataifa ya masula ya mazingira ya Solar Oven Society Africa, imetangaza mpango wa kuokoa maisha ya watu na uharibifu wa mazingira katika barabara iendayo Kijiji cha Samunge kwa kutoa vyoo na gari la kubeba wagonjwa. Akizungumza na Mwananchi jana, Mwakilishi wa Taasisi hiyo hapa nchini, Profesa Solomon Mwenda alisema wamechukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa kuna tatizo la huduma muhimu kwa wagonjwa na uharibifu mkubwa wa mazingira katika eneo hilo ambalo pia ni mapito ya wanyamapori. “Tumekwenda Samunge na tumeona hali ni mbaya sana na ni hatari kwa afya za watu. Tumekuta bado watu wanajisaidia porini, bado chupa tupu na uchafu mwingi unatupwa barabarani hovyo,” alisema Profesa Mwenda. Alisema kazi ya vyoo itaanza Jumanne ijayo na kwamba kila baada ya kilometa moja kutakuwa na choo cha muda. Pia watatoa gari la kubeba wagonjwa, mifuko ya kutunza taka, mahema na maofisa wa mazingira. Mpaka sasa hakuna hata choo kimoja kilichokamilika kujengwa wakati Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imekuwa ikivuna kiasi cha Sh 6.4.milioni kwa siku katika Kijiji cha Samunge. Tayari halmashauri hiyo imetia kibindoni kiasi cha Sh 140.8 milioni kwa mwezi mmoja lakini hivi sasa kuna taarifa ya mgonjwa mmoja kuhara damu, kwa mujibu wa ripoti kutoka zahanati ya kijiji jicho. Pato hilo linatokana na tozo la ushuru wa kila siku kwa magari yanayokwenda kwa Mchungaji Mwaisapile kwa ajili ya kupata tiba. Mabasi makubwa na malori yanatozwa Sh10,000 kila moja, mabasi madogo yanatozwa Sh5,000 na madogo Sh2,000 huku pikipiki zikitozwa Sh1,000. Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka kijijini, hapo pamoja na pato hilo ambalo awali lilikuwa likikusanywa na kijiji hicho hali bado ni mbaya na uchafu umekidhiri kila mahali vinyesi, mikojo katika chupa za plastiki ni hali ya kawaida eneo hilo . Hali inazidi kuwa mbaya kiafya kutokana na mvua ziloanza kunyesha huku misururu mirefu inayofikia umbali wa kilomita 28 na watu waoadiriwa kufikia 150,000 wakiwa wanasubiri kupata tiba. Msururu huo unaanzia katika Kijiji cha Mdito. Wananchi waliokwama katika msururu huo wamekuwa wakihangaika kupata chakula na vinywaji kiasi kwamba kila abiria wanaopita kutoka Kijiji cha Samunge, wamekuwa wakiombwa maji ya kunywa bila kujali kama yametumiwa na wengine au la. Kijiji cha Mdito chenye kaya zisizozidi 50 hivi sasa kina watu wanaokadiriwa kufikia 200,000 ambao hawana mahitaji muhimu kabisa, huku wengine kama hao wakipata walau huduma kidogo na hao ni wale walio katibu na Kijiji cha Samunge, umbali wa kilometa 10. Wakati huohuo; mvua zinaendelea kunyesha wilayani Ngorongoro hali ambayo inatishia uharibufu wa barabara. Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali alisema kuwa kutokana na mvua hizo, ukarabati wa barabara ambao ulikuwa unafanywa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) umesitishwa kwa muda. “Ni kweli barabara ni mbaya kutokana na mvua, watu wa Tanroads walikuwa wanatengeneza barabara ila nadhani sasa imekuwa kazi ngumu kwani mvua zimewakuta,” alisema Lali. Tangu kuanza kwa mvua hizo takriban wiki moja sasa, mamia ya watu na magari wamekwama katikati ya Kijiji cha Selela na Ngaresero kutokana na mito kujaa na maeneo mengi kuharibika. Lipumba aiponda Serikali Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameishukia Serikali kwa kuruhusu tiba hiyo bila kufanyiwa uchunguzi na mkemia wake mkuu. Lipumba ambaye hata hivyo, katika maelezo hayo hakuwakatisha tamaa wananchi kwenda kupata tiba hiyo, alisema kiutaratibu, watu hawazuiliwi kufanya tiba, lakini dawa lazima zipite kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili athibitishe ubora wake kabla ya kuruhusu watu waanze kuitumia. Profesa Lipumba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Viwanja vya Zakheim, Mbagala Dar es Salaam. "Katiba yetu haizuii mtu kuendesha shughuli za tiba, lakini taratibu ni kwamba tiba lazima ithibitishwe na maabara za Serikali. Ukiona Serikali inawaruhusu watu kutumia tiba bila kufuata utaratibu huo ujue imekwama," alisema. Ingawa Lipumba hakutaja moja kwa moja tiba ya Loliondo, tiba iliyoanza kutolewa katika siku za hivi karibuni na kuibua mjadala mkubwa miongoni mwa jamii ni ile inayotolewa na Mchungaji Mwasapile. Profesa Lipumba aliponda uamuzi wa Waziri Lukuvi kushinikiza tiba hiyo itolewe bila vipimo akisema ni sawa na kuhalalisha mambo yaendee kiholela katika nchi ambayo imejiwekea utaratibu wake kisheria. "Waziri wa afya alikuwa sahihi sana kutaka dawa hiyo ipimwe kwanza, lakini Lukuvi akapingana naye, hii ni dalili mbaya kwa Serikali," alisema. Habari hii imeandaliwa na Filbert Rweyemamu, Moses Mashala, Emanuel Herman, Arusha na Kizitto Noya. |
Last Updated on Saturday, 26 March 2011 08:36 |
Add comment
Taarifa Maalum |
Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
Kupiga Kura
Jumapili
Comments
Quoting Pengo Jr:
Pengo jr soma hoja nzima ya kadinali Pengo. usisome mstari mmoja halafu ukatoa conclusion. wewe unasema Pengo hajampinga babu. Je aliposema:"Miujiza haiji kwa urahisi hivyo na watu kuponya kiasi hicho, huenda wanaweza kuponywa kwa ‘Illusion’ na baade ikaleta madhara" alikua anamsapoti
Ni kweli Ngosha.
#60 Rehema-Nilikaribia kukubaliana nawewe ila sijaona connection na shetani hapo. Hakuna concrete point kuunganisha na shetani.
#53 shebby-Just a mere assumption. Unataka tuamini ama tukubali?
#47 kunicha-Usimuite babu tapeli kwakuwa hafanyi unavyotaka wewe please.
#45 abdy-Huna fact za msingi. Hata neno can be dawa. Sio kikombe tu.
#34 kiongozi-Hoja za Pengo ni pumba tupu-Zako nzuri ziko wapi?
#23 Embu-Pengo hana mkate wowote. Hana dhiki kama wewe. Amesema hana uhakika na uponyaji wa watu wengi kama hivyo. Sio kaponda.
#18 msema kweli daima-I guess akili na ushujaa wako ni kuumwa na sioni busara kwako.
#16 MWANAMDODO-Sio lazima wote tuamini. Tumia busara
Pengo alisema ““Ila sina jibu la kutoa kuhusu uponyaji huo, nabaki tu kushangaa na yanayotendeka kwa Mchungaji huyo hadi kufikia watu kuamini kiasi hicho” Hakuponda, hakukataa.
NI RAHISI KUMSAFIRISHA YEYE MIKOA MBALIMBALI, KULIKO WATANZANIA WOOOOOOOTE WAMFUATE YEYE HOKO LOLIONDO!
SERIKALI HAIJATUMIA BUSARA KATIKA HILI!
SHERIA ZA AFYA NA USALAMA WA RAIA ZINAKANYAGWA - KWA VILE HAKUNA ANAYESIMAMIA SHERIA TANZANIA.
HIVI KWELI KILA MTU AKIFANYA HIVI TUTAISHIJE WATANZANIA?
KESHO MWINGINE AKITUAMBIA YESU YUKO KATIKATI YA BAHARI YA HINDI TUTAKIMBILIA HUKO?
KAMA MTU ANA DAWA, AFUNGUE ZAHANATI NA HOSPITALI ZAKE KWA KUFUATA UTARATIBU JAMANI.
TUTAACHAJE KUAMINI KUWA WATU WANAENDA KUTAFUTA MADARAKA KWA WACHAWI, WAGANGA WA KIENYEJI NA WANAJIMU?
Hili dili nyie subirini tu litabumburuka muda si mrefu. Serikali itaingia aibu ya mwaka kwa kuwa inaingilia kitu cha hovyo. Serikali imetoa kibali kila anayeota sasa atibu watu! Serikali ya hovyo kabisa! Eti inaogopa kuchukiwa na walokole! kwani sasa wanaipenda serikali! Serikali inayotafuta baraka za mtu aliyeota! Kha! Inatia kichefuchefu. Jamani, uchauzi ujao chagueni mtu makini. Mkichagua mhuni mtapata mambo ya kihuni kama haya. Ingekuwa mwalimu yupo hai akiwatia bakora hao japokuwa ni wakristu wenzie.
mnatuchanganya babu anatibu au anaponya tucheck kamusi hakafu mtuweke wazi...
Please hii habari ilikuwa katika gazeti la Habari leo tuesday or wednesday. Weka ukulasa wa juu ili aone kuna comments ngapi maana wanasoma
Jamani mimi nilidhani ni Magazeti (Print) tuu huwa yanachelewa kuwafikia wasomaji, sikujua kuwa hata web pages huwa zinachelewa pia, maana it looks like mwenzetu anasoma gazeti la mwezi uliopita.. this is worth looking into, or it could be ndiyo amefunga modem yake hivyo ameanzia kwenye ARCHIVES, strangely comments came to the wrong forum of comments.. TECHNOLOGY!!!!!